Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kanisa Kuu RC Geita lafungwa kwa muda

Kanisa Kuu Jimbo Katoliki Geita. Picha na Rehema Matowo

Muktasari:

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita, Flavian Kassala ametangaza kulifunga kwa muda usiojulikana Kanisa Kuu la jimbo hilo lililoko mjini Geita siku chache baada ya kijana aliyewahi kuwa muumini wa kanisa hilo kuvamia na kuharibu vifaa na maeneo matakatika ikiwemo mimbari (altare), kiti cha Kiaskofu na vyombo vya sakramaenti.

Geita. Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Flavian Kassala ametangaza kufungwa kwa muda usiojulikana Kanisa Kuu la jimbo hilo lililoko mjini Geita lililovamiwa na kuharibiwa vifaa na maeneo matakatifu ikiwemo mimbari (Altare), kiti cha Kiaskofu na vyombo vya sakramenti.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumanne Fevruari 28, 2023, Askofu Kassala amesema kanisa hilo ambako ndiko pia yaliko makazi ya Kiaskofu limefungwa rasmi kuanzia jana Jumatatu Februari 27, mwaka huu.

“Ni kweli Kanisa limefungwa kuanzia jana Jumatatu Februari 27, 2023; uamuzi huu umetokana na kufuru na unajisi uliofanyika ndani ya Kanisa  ikiwemo maeneo matakatifu kiimani,” amesema Askofu Kassala

Akifafanua, kiongozi huyo wa Kiroho amesema tukio la uvamizi na uharibifu wa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu umenajisi utakatifu siyo tu wa vifaa mbalimbali vya ibada, bali pia jengo lote la kanisa.

“Kiimani, tukio la uvamizi na uharibifu ndani ya Kanisa Kuu Jimbo la Geita ni kufuru kubwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu; tukio lile limeivunjia heshima Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, imeathiri na kuumiza imani yetu kwa kiasi kikubwa sana,” amesema

Amesema kutokana na yote yaliyotendeka, Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita halistahili kwa maadhimisho ya Sakramenti ya Ekaristi yoyote wala ibada ya aina yoyote.

Akizungumza kwa sharti la kuhifadhiwa jina, mmoja wa viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza amesema kiimani, Kanisa Kuu la Geita litahitaji kubarikiwa upya kabla ya kuanza kutumika tena kwa sababu uvamizi na uharibifu wa maeneo matakatifu uliofanyika umeondoa baraka wakfu wake.

“Kiimani, kanisani kuna maeneo matakatifu ambayo watu hawayafikii kiholela; kitendo cha kuvunja altare (mimbari), kuvunja misalaba na eneo la ekaristi siyo tu ni laana kwa aliyehusika, bali pia ni kufuru inayohitaji ibada maalum ya utakaso ba Baraka,” amesema kiongozi huyo

Tukio lilivyotokea

Tukio la uvamizi Kaanisa hilo lilitokea Saa 8:00 usiku wa kuamkia Jumapili Februari 26, 2023 na kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo, kijana aliyehusika (jina linahifadhiwa) amebainika kuwa ni muumini aliyewahi pia kuwa mhudumu kanisani hapo.

Kamanda huyo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyo alikuwa amelewa wakati anavamia na kufanya uharibifu kanisani hapo kutokana uchunguzi wa kitabibu kubabaini kiwango kikubwa cha kilevi mwilini mwake.

Amesema kabla ya kuvamia na kuharibu mali kanisani, kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 alionekana Baa akinywa pombe hadi Saa 7:00 usiku akiwa na wenzake watatu.

Kijana huyo aliyeingia eneo la Kanisa kwa kuvunja kioo cha lango kuu anadaiwa kuvunja altare, kiti cha Kiaskofu, misalaba, sanamu mbalimbali za kiimani na vyombo vya kuhifadhia ya maji ya baraka ambayo pia aliyamwaga.