Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dorothy Semu alivyozuiwa kuingia Kisutu

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amejikuta kwenye majibizano na askari wa Jeshi la Polisi akiwa nje ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Semu alikuwa mahakamani hapo leo Alhamisi, Aprili 24, 2025 ambapo kesi mbili ya uhaini na ile ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni zinazomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu zinasikilizwa.

Akiwa nje ya geti la Mahakama hiyo, upande wa uelekeo wa mataa ya Ohio, Semu alishuka kwenye gari lake kwa lengo la kuzungumza na wanahabari.

Askari watatu wa kike wa kutuliza ghasia walimzuia wakitaka aondoke eneo hilo.

Kiongozi huyo alikataa na kudai eneo hilo si la Mahakama, hivyo  amesimama kihalali na kutaka asilazimishwe kuondoka.

Wakati mvutano huo ukiendelea, askari wengine zaidi ya saba wanaume wakiwa kwenye gari ya Polisi walisogea kwenye kusanyiko hilo bila kuzungumza chochote huku wawili kati yao wakishuka na kutawanya kusanyiko hilo kwa kuwatishia mbwa,  Semu na waandishi wa habari.

Wakati wakifanya hivyo, mmoja wa viongozi wa ACT Wazalendo aliwafokea askari akiwatuhumu kuwatishia mbwa na kumfungulia kiongozi huyo mlango wa gari ili apande waondoke.

Waandishi pia walikimbia kukwepa kudhuriwa na mbwa hao wa Polisi kabla ya Semu kuondoka eneo hilo saa 5:25 asubuhi.

Baada ya Semu kuondoka, askari wenye mbwa nao walisogea upande mwingine kuendelea na majukumu yao, huku waandishi wa habari wakikimbilia kwenye korido za majengo yaliyo jirani na Mahakama hiyo.

Wakati huo mvua ilikuwa imeanza kunyesha katika viunga hivyo kwa Mahakama ya Kisutu.


Endelea kufuatilia Mwananchi