Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Janet Magufuli mgonjwa

Janeth Magufuli

Dar es Salaam. Joseph mtoto wa rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli amesema mama yake,  Janet anaendelea na matibabu baada ya kupata mshtuko kufuatia kifo cha mumewe.

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Magufuli wakati wa kongamano la viongozi wa dini, Joseph amesema mama yake hayupo vizuri kiafya lakini anaendelea na matibabu.

“Mama hakuweza kuja kwa sababu ya tatizo la kiafya alipatwa na mshtuko baada ya baba kufariki, yupo anaendelea na matibabu."

"Mama anawashukuru viongozi wa dini na watu wote kwa kuliombea Taifa wakati wote wa msiba na ilikuwa jambo gumu kumpoteza mzazi na kiongozi wa Taifa,” amesema.

Joseph amewasisitiza Watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili upendo, amani na mshikamano viendelee kutawala nchini.