Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jaji Chande kuongoza majaji kutazama kesi ya uchaguzi Kenya

Jaji Chande kuongoza majaji kutazama kesi ya uchaguzi Kenya

Muktasari:

  • Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amewasili nchini Kenya kwa ajili ya kuongoza jopo la majaji wengine wa Afrika kutoka katika Jukwaa la Majaji na Wanasheria Afrika watakuwa na kazi ya kutazama mwenendo wa kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 9, 2022.


Dar es Salaam. Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amewasili nchini Kenya kwa ajili ya kuongoza jopo la majaji wengine wa Afrika kutoka katika Jukwaa la Majaji na Wanasheria Afrika watakuwa na kazi ya kutazama mwenendo wa kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 9, 2022.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa Kenya Kwanza William Ruto alitangazwa mshindi kwa kupata kura milioni 7.1 akifuatiwa na mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga aliyepata kura milioni 6.9

Hata hivyo Odinga amefungua kesi Mahakama ya Juu ya Milimani akipinga matokeo hayo akidai kulikuwa na udanganyifu ulioratibiwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya chini ya Mwenyekiti wake Wafula Chebukati.

Chande ameongozana na ujumbe wa wanasheria mashuhuri Afrika ambao ni Lilian Tibatemwa-Ekirikubinza kutoka Mahakama ya Juu ya Uganda, Ivy Kamanga kutoka Mahakama ya juu ya Rufaa ya Malawi, Moses Chinhengo kutoka mahakama ya juu ya rufaa ya Lesotho na Rais wa mahakama ya uchaguzi ya Afrika kusini, Henry Mbha.

Jopo hilo la wanasheria mashuhuri litahudhuria vipindi vyote vya kusikiliza kesi hizo za uchaguzi na watakuwa na haki ya kuchukua nakala zinazohusiana na kesi hizo kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu na usawa.

Pia watachanganua jukumu na uhuru wa Idara ya Mahakama ya Kenya katika kuchunguza mizozo ya uchaguzi. Timu hiyo pia itapitia hali ya kijamii na kisiasa katika maandalizi ya maombi hayo ya kesi za uchaguzi ambazo zimefunguliwa nchini humo.

Kesi nane za kupinga matokeo ya Rais nchini Kenya zimewasilishwa kwenye Mahakama ya Juu ya Milimani huku mahakama hiyo ikitarajia kuanza kuzisikiliza kesi hizo kuanzia Septemba 5, 2022.