Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujenzi ghorofa la vyumba 101 watumishi Dar wafika hapa

Muktasari:

  • Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanakuwa katika makazi bora.

Dar es Salaam. Katika juhudi za kuboresha mazingira ya kazi na maisha ya watumishi wa umma, ujenzi wa jengo la makazi lenye vyumba 101 umeanza jijini Dar es Salaam, likiwa ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuwapatia watumishi makazi bora karibu na maeneo yao ya kazi.

Mradi huo unatekelezwa na Mfuko wa Watumishi Housing Investment (WHI), ukiwalenga watumishi wa kada mbalimbali ndani ya Serikali, hadi sasa ujenzi huo umefika asilimia 20.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa mfuko huo, lengo ni kupunguza changamoto ya upatikanaji wa nyumba za bei nafuu kwa watumishi wa serikali katika Jiji la Dar es Salaam ambako gharama za makazi zinaendelea kupanda.

Hayo yamezungumzwa hivi karibuni na Mgurugenzi Mtendaji wa WHI, Sephania Solomon wakati wa ukaguzi wa jengo hilo lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo la ghorofa linatarajiwa kuwa na vyumba 101 ambapo watumishi watauziwa kwa malipo ya kidogo kidogo endapo akimaliza malipo atakabidhiwa nyumba yake kwa utaratibu maalumu uliowekwa.

“Tunaamini kwa kuwapatia watumishi makazi bora, tutaongeza ari ya kazi na kupunguza muda wanaotumia kusafiri kutoka makazi ya mbali kwenda kazini,” amesema Solomon.

Sambamba na hayo Solomon amesema ameridhishwa na hatua ya ujenzi ulipofikia kwani anaamini mkandarasi huyo atamaliza ujenzi huo kwa muda waliokubaliana.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi WHI, Selestin Muganga amesema ujenzi huo unagharimu Sh18 bilioni ambapo hela yote inatolewa na mfuko huo.

"Ujenzi wa jengo hili unagharimu kiasi cha Sh18 bilioni hela hiyo inatoka kwenye mfuko wa Watumishi Housing Investment, na fedha nyingine kuna watumishi washaanza kulipa pia tunaijumlisha kwenye ujenzi," amesema Muganga.

Amesema ingawa nyumba hazijaisha ujenzi wake lakini tayari nyumba zote zimechukuliwa na watumishi wa serikali kwa nyumba zote 101.

Meneja Mradi, Yusuph Mlimakifi amesema mwitikio ni mkubwa kwa watumishi hivyo atajadiliana na kamati yake kuona kama itawezekana kuwauzia watumishi wengine kutoka sekta mbalimbali hapa nchini.

Ujenzi huo ulianza Septemba 2024 unatarajiwa kukamilika Machi 2026.