Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yathibitisha kumuhoji Mwijaku, wanafunzi waliomshambulia mwenzao

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limethibitisha kuwahoji Mwemba Burton Mwemba, maarufu Mwijaku na wanafunzi wanne wanaidaiwa kushiriki katika tukio la kumshambulia na kumdhalilisha Magnificat Barnabas Kimario ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi.

Katika taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 24, 2025, polisi wameeleza kuwa  hadi sasa watu wanne  wamekamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo ambalo limelaaniwa vikali na jamii.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Maofisa wa Maendeleo ya Jamii, Idara ya Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, linaendelea na uchunguzi wa tukio la  kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Magnificat Barnabas Kimario,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, watuhumiwa hao ni Mary Gervas Matogoro,  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ryner Ponci Mkwawili,  mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, Dar es Salaam, Asha Suleiman Juma,  mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam na Mwemba Burton Mwemba, maarufu  Mwijaku , mkazi wa Dar es Salaam.

“Upelelezi wa shauri hili upo katika hatua za mwisho na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitafuatwa  dhidi ya wote waliohusika,” imeeleza taarifa hiyo.