Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa ajira 11,515 wahudumu wa afya ngazi ya jamii

Waziri wa Afya, Jenista  Mhagama akizungumza jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Watoa huduma hao 11,515 watakaoanza mafunzo Septemba 30 mwaka huu, wanapelekwa katika vituo mbalimbali vya afya kwa kipindi cha miezi sita kabla hawajaanza kutoa huduma za afua jumuishi za afya, lishe na ustawi wa jamii.

Dar es Salaam. Jumla ya watoa huduma ngazi ya jamii 11,515 wanatarajiwa kuanza mafunzo Septemba 30, 2024 ili kufanikisha azma ya mpango jumuishi wa wahudumu hao na kuendeleza afua jumuishi za afya, lishe na ustawi wa jamii.

Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -Tamisemi sambamba na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) wanatarajia kutoa mafunzo hayo yatakayowajenga kwenda kuhudumia Watanzania nyumba kwa nyumba.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 19, 2024 na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama wakati akitoa taarifa kwa umma juu ya kuanza rasmi kwa mafunzo ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa mikoa 11 ya Tanzania Bara.

Waziri Mhagama amesema mpango huo utaanza kwenye halmashauri 21 ndani ya mikoa 11 katika awamu ya kwanza.

“Mikoa ambayo itafikiwa na huduma hii kwa awamu ya kwanza ni pamoja na Geita, Pwani, Tanga, Songwe, Mbeya, Lindi, Tabora, Kagera, Njombe, Ruvuma, na Kigoma," ameainisha na kuongeza;

"Mpango huu umelenga na unahitaji kuwa na wahudumu wawili yaani mwanamke na mwanaume kila mtaa na kila kitongoji, uchaguzi wa wahudumu hao umeshirikisha wananchi na wana jamii kutoka kitongoji husika au mtaa husika,” amefafanua Waziri Mhagama.

Wakati wa utoaji wa mafunzo amesema yatatolewa kupitia vyuo vya afya vya kada ya kati kwa kipindi cha miezi sita, ambapo miezi mitatu ya awali mafunzo yatatolewa kwa njia ya nadharia na miezi mitatu iliyobaki mafunzo yatakuwa kwa njia ya vitendo katika maeneo yao ili kuongeza umahiri kwa wahudumu kuweza kutekeleza kwa uhalisia kile walichojifunza.

Waziri Mhagama amesema jumla ya wanajamii 31,275 walijitokeza kuomba nafasi huku wanajamii 21,574 waliokidhi vigezo kwenye hatua ya awali walichaguliwa.

“Kwa awamu ya kwanza zoezi la kuwachagua wahudumu wa afya ngazi ya jamii lilifanyika kati ya Juni 8 hadi Julai 25, 2024 kwenye halmashauri 21 kwa mikoa kumi na kuleta idadi ya waliokidhi vigezo 21,574 na huku Mkoa wa Ruvuma wahudumu 1,227 wanachaguliwa ili kuwa na jumla ya wahudumu 11,515,” amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama hakusita kuonya wale wote watakaotaka kujinufaisha na zoezi hilo na kuonya kuwa Wizara ya Afya itachukua hatua kali kwa yeyote atakaejaribu kutengeneza mavazi ambayo yatakuwa sawa na mavazi ambayo watayatumia wahudumu wetu na kujifanya ni wahudumu wa afya,” amesema Waziri Mhagama.

Mpango huu ulihusisha jumla ya mitaa 1,044, vijiji 754 na vitongoji 3,853 baada ya uchaguzi kupitia mikutano ya jamii jumla ya wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 9,492 walichaguliwa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dk Ellen Senkoro amesema wamekuwa na ushirikiano na Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa miaka 18 sasa.

Amesema katika mradi huo walikuwa sehemu ya maandalizi ya mpango wa kitaifa na pia wamekuwa wakiwashirikisha kutoa ushauri wa kitaalamu kutokana na majaribio waliyoanza kuyafanya miaka saba iliyopita.

“Huu ni mkakati wa kitaifa kwa ajili ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii na sisi ni sehemu ya kushirikiana nao, kuwatambua na kuhakikisha wanapata mafunzo na stahiki zao kwa wakati.

“Tumepokea maelekezo ya Waziri sasa tukajikite kuhakikisha wanapata mafunzo miezi sita na wakitoka wanakwenda kuhudumia jamii, awamu ya kwanza tutawasimamia kuhakikisha wanapata mafunzo tutashirikiana kwa pamoja, tunashkuru wahisani wameweka fedha na Serikali nayo imeweka fedha,” amesema Dk Senkoro.