Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maelfu wanaoomba ajira waweka wazi ukubwa wa tatizo

Muktasari:

  • Naibu Waziri Deus Sangu amesema Serikali haiwezi kuajiri vijana wote waliomaliza vyuo kutokana na bajeti ndogo, akisisitiza haki na uadilifu katika mchakato wa usaili wa ajira za afya.

Dar es Salaam. Suala la ukosefu wa ajira ni tatizo la kimataifa, lakini hali ni mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea kutokana na upungufu wa fursa za kazi licha ya idadi kubwa ya waombaji.

Kwa mfano, katika ajira zilizotangazwa Julai 20, 2024, nafasi 12,000 za kada ya afya zilitangazwa, lakini zaidi ya watu 47,000 waliomba. Upande wa walimu, waombaji walifikia 200,000, ingawa waliotakiwa ni 11,015.

Akizungumza leo Septemba 11, 2024 jijini Arusha, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, amesema vijana wengi wamemaliza vyuo na wako mtaani, lakini kutokana na bajeti ya Serikali na hali ya uchumi, haiwezekani kuajiri vijana wote waliomaliza vyuo.

Sangu alikuwa anazungumza na wataalamu walioteuliwa kuendesha usaili wa ana kwa ana kwa wasailiwa wa kada ya afya katika mikoa mbalimbali nchini.

Aidha, Sangu amewataka wanajopo wa usaili kuwa waadilifu na kuhakikisha haki inatendeka kwa kila msailiwa, akisisitiza kuwa ajira ni suala la usalama wa nchi.

Ameonya kuwa yeyote atakayevuruga mchakato wa usaili atakutana na matatizo makubwa.


"Tunatafuta vijana watakaoingia serikalini kwa utumishi wa umma kwa miaka isiyopungua 25. Tukifanya makosa na kupeleka vijana wasio na sifa tutaligharimu Taifa kwa zaidi ya miaka 25," alisema Sangu.

Pia amewataka wanajopo kuepuka upendeleo na kutenda haki katika maamuzi yao.

Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Samuel Tanguye, amesema mchakato huo unalenga kupata vijana wenye weledi watakaosaidia Taifa.