Haya hapa majina walioitwa usaili ajira za TRA

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza majina ya waliochaguliwa kufanya usaili wa nafasi mbalimbali za kazi zilizotangwa kuanzia Februari 6 hadi 19 mwaka huu.
Tangazo hilo lililotolewa na Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala ya TRA imesema kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kwa hatua mbalimbali kuanzia Machi 29, 2025.
Taarifa ya kuitwa kwenye usali huo imetangazwa leo Jumamosi Machi 22, 2025 katika tovuti na mitandao mbalimbali ya TRA.