Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GGML yasaini mkataba wa uuzaji Dhahabu na Benki Kuu ya Tanzania

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba,  pamoja na Duran Archery, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited baada ya kusaini Mkataba wa Kwanza wa Uuzaji wa Dhahabu na kampuni kubwa ya uchimbaji madini, katika makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyopo Dodoma.

Dodoma. Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), inayomilikiwa na AngloGold Ashanti, imesaini mkataba wa huduma ya uuzaji dhahabu na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na kuwa kampuni ya kwanza ya uchimbaji mkubwa nchini kutekeleza agizo la kisheria chini ya Kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini.

Mkataba huo, uliosainiwa katika makao makuu ya BoT jijini Dodoma, unairuhusu GGML kuuza asilimia 20 ya dhahabu yake kwa Serikali kupitia Kiwanda cha Usafishaji Dhahabu cha Geita (GGR). Mpango huu unahakikisha upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya ndani vya usafishaji, hatua muhimu katika kufikia viwango vya kimataifa kama vile uidhinishwaji wa London Bullion Market Association (LBMA).

Kwa kusambaza sehemu ya uzalishaji wake kupitia kiwanda cha ndani, GGML inachangia juhudi za Serikali za kuimarisha thamani ya shilingi na kukuza fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania wanaojihusisha na usafishaji na uongezaji thamani madini.

Akizungumza wakati wa tukio la utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Duran Archery amesema:

“Tunafurahia kushiriki katika hatua hii muhimu. Ni mfano wa wazi wa namna sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali kuimarisha viwanda vya ndani na kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.”

Mkataba huu ni matokeo ya mashauriano ya kina kati ya GGML, Benki Kuu ya Tanzania na Wizara ya Madini. Ni hatua muhimu katika utekelezaji wa sera za ushirikishaji wa waTanzania na mkakati wa kitaifa wa kuongeza thamani ya madini