Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Doreen wa Lucky Vincent, afanyiwa upasuaji mdogo kuondoa vyuma

Muktasari:

  • Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook na kueleza kuwa Doreen amepata nafuu kubwa na sasa anatarajiwa kupelekwa katika matibabu maalum ya uti wa mgongo, Nebraska, Lincoln.

Sioux. Manusura wa ajali ya basi la Shule ya Msingi, Lucky Vincent, Doreen Mshana, amefanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa vyuma vilivyowekwa wakati alipofanyiwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo, taya na nyonga.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook na kueleza kuwa Doreen amepata nafuu kubwa na sasa anatarajiwa kupelekwa katika matibabu maalum ya uti wa mgongo, Nebraska, Lincoln.

“Madaktari wataamua aende lini baada ya kuondolewa vyuma,  tuendelee kumwombea apone katika changamoto alizonazo,” ameandika Nyalandu.

Doreen na wanafunzi wengine wawili, Saidia Ismael na Wilson Tarimo walinusurika katika ajali hiyo iliyotokea Mei 6 na kuua wanafunzi wenzao 32 , walimu wawili na dereva.