Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deni la Sh4.9 bilioni la ATCL lasababisha wastaafu kukosa haki zao

Muktasari:

  • Serikali imetaja chanzo cha kutolipwa kwa wastaafu wa ATCL ni madeni ya Sh4.9 bilioni zinazotokana na kutowasilishwa kwa michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Dodoma. Serikali imetaja chanzo cha kutolipwa kwa wastaafu wa ATCL ni madeni ya Sh4.9 bilioni zinazotokana na kutowasilishwa kwa michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Februari 6, 2023 na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete na akasema fedha hizo zimepangwa kulipwa katika bajeti ya 2022/23.

Mwakibete ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalumu Angelina Malembeka (CCM).

Katika swali lake mbunge huyo amehoji ni lini Wastaafu wa ATCL watalipwa mafao yao ambayo wamekuwa wakiidai Serikali kwa muda mrefu.

Mwakibete amesema kabla ya kuanza kuifufua ATCL Septemba 2016 ilikuwa ikikabiliwa na changamoto za uendeshaji kwa kukosa mtaji, kuwa na ndege mbovu, kushindwa kulipa madeni ya wazabuni na kutowasilishwa michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Kwa kuzingatia uhakiki uliofanyika, ATCL ina madeni ya zaidi ya Sh4.86 bilioni yanayotokana na kutowasilishwa michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii," amesema Mwakibete.

Amesema tangu 2016 fedha za mifuko zinapelekwa hivyo madeni hayo ya michango yamepangwa kulipwa mwaka huu wa Fedha.