Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deni la Serikali lafikia Sh79.1 trilioni hadi Machi 2023

Muktasari:

  • Deni la Taifa limeendelea kuongezeka sababu ikitajwa kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji.

Dodoma. Serikali imesema kuwa mpaka Aprili mwaka huu, deni lake limefikia Sh79.1 trilioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.9 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Bungeni na waziri mwenye dhamana ya fedha na mipango wakati wa uwasilishaji wa Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2023/24 kati ya deni hilo, la nje ni Sh51.16 trilioni huku lile la ndani ni Sh27.93 trilioni.

Waziri Mwigulu Nchemba amesaema ongezelo hilo lilitokana na kuongezeka kwa mahitaji ya fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya.

Aidha amesema hadi kufikia Machi 2023, Serikali ilikuwa imekopa Sh1.3 trilioni kutoka vyanzo vya nje vyenye masharti ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo, bunge limeelezwa leo.