DC Mpogolo ataka kila shule Ilala iwe na klabu ya kodi

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo
Muktasari:
- Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amemtaka Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Charangwa Makwiro kumwandikia barua mkurugenzi wa jiji kuhakikisha shule zote za sekondari ziwe na klabu za Kodi.
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amemtaka Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Charangwa Makwiro kumwandikia barua mkurugenzi wa jiji kuhakikisha shule zote za sekondari ziwe na klabu za Kodi.
Akizungumza hayo leo Septemba 27, 2023 katika mashindano ya vilabu vya kodi vinavyosimamiwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) vilivyofanyika katika shule ya sekondari ya Jamuhuri amesema yeye ni mlezi hatahakikisha vilabu vya kodi zinaanzishwa katika shule zote za sekondari za jijini humo
Amesema Serikali inachaguliwa na wananchi ili kuwafanyia maendeleo mbalimbali ikiwemo kujenga shule hivyo vilabu hivyo ni muhimu kuanzishwa lengo lao kuwajengea uelewa dhidi ya mlipa kodi na wanapoenda kununua bidhaa yeyote wanatakiwa kudai risiti.
"Kwa kuwa mimi ni mwenyekiti na pia ni mlezi wa hizi vilabubahati nzuri Mkuu wa wilaya anaingia Kila sehemu ikiwemo kwenye vyama mbalimbali kama kwenye chama cha waganga wa jadi, wafanyabiashara Kwa kuwa mimi ni mlezi na ni mshauri," amesema Mpogolo.
Amesema katika wilaya hiyo wanatarajia kujenga shule za ghorofa nane za sekondari kati ya hizo moja itajengwa katika shule ya sekondari ya Jamuhuri ambayo itagharimu kiasi cha Sh1.3 bilioni.
Naye Naibu Kamishna wa kodi za ndani nchini, Edmund Kawamala amesema wanufaika wa kodi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwahimiza watu wanaponunua vitu mbalimbali wapewe risiti ya mashine ya EFD kwa kuwa Serikali inalipa mishahara na inafafnya maendeleo mbalimbali kama ujenzi wa hospitali, zahanati, shule na Kulipa mishahara kwa wafanyakazi wa imma.