Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CWT kwa moto, nani kuibuka mshindi kiti cha urais kesho

Muktasari:

  • Uchaguzi wa Chama cha Walimu hufanyika mara moja kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo mara ya mwisho ulifanyika Mei 2020 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Dodoma. Ni mtifuano, ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kampeni kali zinazoendelea katika Jiji la Dodoma wakati uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) ukitaraji kufanyika kesho Jumatatu Juni 9, 2025.

Wajumbe wa CWT kutoka Tanzania Bara watawachagua viongozi wao huku wagombea 153 watapambania nafasi nane.

Nafasi zinazogombaniwa ni ya rais wa CWT inayowaniwa na wagombea 18, makamu wa rais (19), katibu mkuu (4), naibu katibu mkuu (15), mweka hazina wagombea saba, mwakilishi wanawake wagombea wanne, mwakilishi wenye ulemavu watano, kundi la vijana tisa na upande wa wadhamini wameomba wagombea 52.

Chama hicho kinafanya uchaguzi kikiwa kimepita kwenye milima na mabonde huku viongozi waliochaguliwa miaka mitano iliyopita, amebaki rais, Leah Ulaya pekee huku nafasi ya Katibu Mkuu ikiwa imeshikwa na watu watatu tangu wakati huo baada ya wengine kuingia katika migogoro na kuondolewa.

Hata hivyo, ushindani mkali upo kwa nafasi ya rais, vigogo wakuu wameomba nafasi hiyo huku ikielezwa ni mbinu zitakazoamua nani atapenya.

Rais wa sasa wa CWT, Ulaya na makamu wake, Suleman Ikomba ni miongoni mwa walimu 18 walioomba nafasi hiyo na kufanya ushindani kuwa mkali ambapo wanawake wapo watatu huku wanaume wakiwa 15.

“Tangu tumeanza uchaguzi wa chama hiki hakujawahi kutokea makamu wa rais wakaomba nafasi moja na rais wake, hii ni mara ya kwanza, ndiyo maana wajumbe wamegawanyika,” amesema mmoja wa makatibu wa mikoa ya Kaskazini aliyeomba asitajwe jina.

Mmoja wa wagombea katika kiti hicho, James Ndomba amesema ushindani ni mkali, lakini wanaamini wajumbe watawapa nafasi kubwa vijana kwa sababu viongozi wa ngazi ya juu wamekuwa na mvutano ambao huenda utatoa nafasi kwa mgombea mwingine kuibuka.

Ndomba amesema ili kujua kipimo sahihi cha uongozi, kamati ya uchaguzi ilipaswa kuwaita wagombea wote na kuwapa mdahalo kwani wengi wanatajwa kwa majina, lakini akasema uwezo wao unaonekana kuwa ni mdogo wakati mwingine kuliko vijana.

Nafasi nyingine ambayo imekuwa na ushindani ni ya katibu mkuu inayoshikiliwa na Joseph Misalaba anayechuana vikali na Simon Kepha licha ya Jeston Benjamin kuonekana kuwa na nguvu pia Abihudi Bukuku naye akiendelea kuchanja mbuga kwa wajumbe.

Ushindani mwingine kwa mujibu wa wajumbe ni uwakilishi wanawake, wagombea wanne wamejitokeza huku Osmunda Kinyangazi akipewa nafasi kubwa licha ya ushindani kutoka kwa Elizabeth Werema.

Akizungumzia ushindani huo, Kinyangazi amesema hahofii majina ya wakubwa, licha ya kuwa na umri mdogo atahakikisha anapambana hadi tone la mwisho.

Akifungua mkutano huo leo Jumapili, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema Serikali imeendelea kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu kwani ni wazalishaji wa watalaamu mbalimbali waliopo katika sekta zote ikiwemo afya, nishati, sayansi na teknolojia.


Sambamba na kufanya maboresho yatakayowaongezea walimu ari ya kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.


Mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo yanachangiwa moja kwa moja na walimu. Hivyo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kina mchango mkubwa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla kwa kuwa pamoja na jukumu la kufundisha na kujengea watu maarifa, mwalimu ni mzazi wa kiroho, kiongozi wa fikra, na ni mjenzi wa maadili katika jamii.


Dk Biteko akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kuimarisha sekta ya elimu ili kuongeza ufanisi na kusogeza huduma kwa jamii.


Serikali imefanikiwa kujenga jumla ya madarasa 62,685 kwa shule za msingi na sekondari, shule mapya za sekondari 1,031, shule mpya za msingi 1,580 na nyumba za walimu 1,792.


Amesema katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2024/25, Serikali imefanikiwa kuwalipa malimbikizo ya mishahara walimu 101,596, kulipa watumishi 156,556 madeni yasiyo ya mishahara na kuongeza mshahara kwa watumishi wa umma ambapo kima cha chini kuanzia mwezi Julai, 2025 kitakuwa shilini 500,000 badala ya 370,000.


“Serikali inaendelea kutoa ajira za walimu ambapo kuanzia mwaka 2021 hadi sasa, jumla ya walimu 40,527 wameajiriwa katika maeneo mbalimbali nchini. Lengo la kufanya hivi ni kutatua changamoto mbalimbali zilizopo,” amesema Dk Biteko.