Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo, Gavu wahitimisha ziara Rukwa kwa maagizo

Muktasari:

  • Ziara ya siku nne ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho, Issa Ussi Gavu waliyoianza Oktoba 8, 2023 mkoani Rukwa wameihitimisha leo Jumatano kwa mkutano mkubwa wa hadhahara huku wakiutumia kutoa maagizo mbalimbali.

Sumbawanga. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amehitimiza ziara ya siku nne mkoani Rukwa kwa kutoa maagizo kwa Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Maagizo kwa Wizara ya Kilimo ni kuhakikisha wakulima wanaodai fedha za mauzo ya mahindi wanalipwa na kununua waliyonayo haraka iwezekanavyo.

Kwa Tamisemi ni kufuatilia na kuchukua hatua kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya afya na elimu waliyoitembelea mkoani Rukwa inayosuasua.

Chongolo ametoa maagizo hayo leo Jumatano, Oktoba 11, 2023 wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Nelson Mandele, Sumbawanga Mjini, Mkoa wa Rukwa.

Ziara hiyo ilianza Oktoba 8, 2023 akitokea mkoani Katavi ambapo alikagua miradi ya maendeleo, kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Ufumbuzi ni pamoja na kumwita Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratius Ndejembi aliyetumia mkutano huo kutoa maelekezo ya maeneo ambayo ziara ya Chongolo iliyabaini kwenye miradi mbalimbali ya afya na elimu.

Katika mkutano huo, Chongolo ametumia takribani dakika 30 kuhutubia mkutano huo akigusia kero kubwa ya wakulima kutolipwa fedha zao baada ya kuuza mahidi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Chongolo amegusia suala la kilimo akisema mkoa huo unajituma kwa kulima na jukumu la Serikali ni kunyoosha mambo ili kumrahisishia mkulima kufurahia kile anachokifanya.

Amesema kwenye ziara hiyo alikutana na kero hiyo ya NFRA walinunua mazao ya wakulima lakini hawajalipwa na bado wengine wana mahindi hawajayauza.

“Ninaiagiza wizara ya kilimo, wakulima waliouza mazao yao walipwe haraka. Lakini kuna mazao ya mahindi wanayo ndani wanahofia kuuza kwani NFRA wameondoka, naagiza wizara kwenda kununua mahindi hayo haraka,” amesema

Amesema utabiri wa hali ya hewa unaonesha kutakuwa na mvua kubwa El ninyo na hatua hiyo inaweza kusababisha uhaba wa chakula: “kwa maana hiyo, tunaielekeza Serikali kununua chakula cha kutosha ili uhaba ukitokea tuwe na chakula cha kutosha.”

“Suala jingine ni mbolea, msimu uliopita mbolea ilikuwa inapatikana mbali kwa hiyo sasa tunaitaka wizara ya kilimo kuhakikisha inasogeza mbolea karibu zaidi ili iweze kupatikana karibu zaidi kwa wakulima,” amesema huku akishangiliwa

Amesema miradi waliyoikuta na changamoto wizara za kisekta zichukue hatua za haraka na za makusudi ili ziweze kuendelea na kutoa matokeo chanya kwa wananchi

Amesema kwenye elimu na afya licha ya changamoto kuwepo lakini kuna mafanikio makubwa yamefanyika na kuwapunguzia adha wananchi kupata huduma na watoto kutembelea umbali mfupi.

Chongolo amesema suala la umeme maeneo mengi yamefikiwa na kuwataka Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) kufikisha uememe kwenye vijiji vyote kabla ya Desemba lasivyo hatua kwa wahusika zitachukuliwa.

“Rea wametuhakikishia hadi Desemba vijiji vyote vya Rukwa view na umeme, sasa muda huo ukipita umeme haujafika tutaona cha kufanya mbele ya safari kwa hao watakaokuwa wametudanganya,” amesema Chongolo huku akishangiliwa na umati ya watu

Kuhusu usafiri na usafirishaji, Chongolo amesema kulikuwa na meli mbili za Mv Liemba na Mv Mwongozo. Liemba ilifanya kazi zaidi ya miaka 100 na Mwongozo nayo ikafanya imechoka lakini leo Jumatano kuna mkataba unasainiwa Kigoma na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ya ujenzi wa kanakana.

Amesema hatua hiyo ni kwenda kujenga meli ya mizigo zaidi ya tani 3,000, yaani ni sawa na malori zaidi ya 30 au magari 100 madogomadogo na hii ndani ya miaka miwili au mitatu itakuwa historia kwa usafiri kutoka Tanzania kwenda DR Congo, Burundi na au Zambia.

Mtendaji mkuu huyo wa chama tawala amewataka watumishi wenye dhamana ya kuwatumikia wananchi: “kuwahudumia wananchi, kuwasikiliza na kutatua changamoto za wananchi na wakitimiza hilo wananchi hawatakuwa na maswali au manung’uniko yoyote.”

“Tuko timamu na sawasawa, tunawajibu na hatutasita popote tukiona kuna changamoto ili kuchukua hatua.”

Gavu atoa onyo kwa watumishi

Katika ziara hiyo Chongolo ameambatana na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho, Issa Ussi Gavi aliyewaomba Wanaccm na wananchi kuendelea kuwa na imani na mategemeo na chama hicho kwani wameyaweka sehemu sahihi: “chama hiki kimejiandaa kuendelea kushika dola.”

“Sisi kama CCM tutaisimamia, tutaongoza na kuielekeza Serikali ya Jamuahuri ya Muungano wa Tanzania kutekeleza kero na changamoto za wananchi. Katika ziara hii yapo maeneo tumefanya vizuri na yapo maeneo yanasuasua.

“Tuwahakikishie CCM tunakwenda kusimamia vyema miradi tuliyoiona inasuasua na kufanya hivyo ni kuufanya uchaguzi unakuwa rahisi na tutahakikisha Serikali inatekeleza hilo na kama kuna mradi kwenye halmashauri mnauona unasuasua tutausimamia hadi ukamilike,” amesema

Katika kusisitiza hilo, Gavu amesema: “hatuna muda wa kulea mtu, kulea jambo, jukumu tulilopewa ni kuhakikisha tunasimamia vyema na niwatoe hofu CCM imara inakwenda kusimamia miradi hiyo hasa ile inayosuasua mkoani Rukwa.”

Katibu huyo amesema: “sisi kama chama, tutahakikisha aliyepewa dhamana anasimama kwa miguu yake, kusimamia kile alichopewa na hatutamuonea muhari asiyetekeleza majukumu yake ipasavyo.”

Gavu amesema katika uchaguzi mkuu uliopita mkoa huo ulifanya kosa na jimbo la Nkasi Kaskazini wakalipoteza kwa Aida Kenani wa Chadema aliyemshinda mgombea wa CCM, Ally Kessy aliyekuwa akitetea jimbo hilo:”sasa tulifanya makosa, ila uchaguzi ujao tunahitaji jimbo letu na Kata ya Kizwite.”

Tamisemi: Hatutamfumbia macho mtu

Akijibu kero zilizobainika kwenye ziara hiyo, Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratius Ndejembi amesema amepokea bango kitita kuonesha changamoto mbalimbali kwenye ujenzi, umaliziaji wa miradi ya sekta ya afya na elimu na hatua ambazo amekwisha kuzichukua.

Amesema kwa niaba ya Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa: “namwelekeza Katibu Mkuu wa Tamisemi kwa niaba ya waziri wangu wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa kutuma timu ya wataalamu kufuatilia wilaya ya Nkasi, Sumbawanga vijijini na Simbawanga Mjini, miradi yote inayotekelezwa.”

Amesema timu hiyo itafuatilia kuona fedha zilizotolewa na zilivyotekelezwa kweye sekta ya afya ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini na baada ya hapo hatua sitahiki zitachukuliwa kwa wote watakaohusika kufanya ubadhirifu.

“Nikuhakikishie katibu mkuu wetu wa chama, Tamisemi hatutamwonea mtu, kumfumbia macho atakayebainika kufanya makossa haya na timu hii itapitia miradi yote iliyotengewa fedha, Serikali ya Rais Samia haitamwacha mtu achezee miradi ya wananchi,” amesema

“Ofisi ya Tamisemi haitamwacha mtu, tutamchukulia hatua yoyote na hapa Rukwa tumekwisha kuwachukulia hatua watu, niwaambie watumishi wenzetu, tuisimamie miradi hii kwa uadilifu mkubwa, tusiichezee kwani ukibainika hatutakuacha,” amesema

Amesema changamoto ya magari ya wagonjwa kwa baadhi ya halmashauri imepatiwa ufumbuzi kwa fedha kutengwa ili kuhakikisha: “kila halmashauri zote nchini zinapata magari mawili ya wagonjwa na kwa kuanza tutaanza na mkoa wa Rukwa.”

Naibu waziri huyo amesema magari mengine yatakuwa ya mganga mkuu wa mkoa kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa huduma kwenye mkoa wake.

Ndejembi alitoa wito kwa wanganga wakuu wote wa mikoa na wilaya kupanda miti ya matunda katika hospitali, zahanati na vituo vya afya ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Chongolo ambayo amekuwa akiyatoa kila alipopita kukagua miradi ya maendeleo.

Alichokisema Aeshi

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa mkoa huo, Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hilaly alisema tangu ziara hiyo ya Chongolo ilipoanza Oktoba 8 mwaka huu akitoka mkoani Katavi imekuwa na mafanikio,”na naomba tufikishie salamu zetu kwa Rais Samia kuwa tunampenda na mwaka 2025 tuko.”

“Tangu nimekuwa mbunge 2010 hadi leo, hatukuwa na uwanja wa ndege, lakini fedha zimeingia na mkandarasi yuko anaendelea na kazi, hatukuwa na hospitali ya wilaya na sasa tunayo na tunajenga Hospitali ya Rufaa na ikikamilika kila madaktari bingwa watakuwepo,” alisema Aeshi

Alisema wiki mbili zilizopita wamesainia mikataba ya zaidi ya kilomita 16 na wiki mbili zingine watasaini mikataba ya kujenga barabara mbalimbali.

“Sumbawanga tulikuwa na kero kubwa sana ya maji, lakini sasa miradi imekuja na inaendelea na maeneo mengine yanapatikana na baada ya muda mfupi kero ya maji itakuwa baibai,” alisema.

Aeshi amesema wamejenga vituo vya afya katika kata zote na mpaka sasa kata nne zimejenga na bado tatu na kabla ya uchaguzi mkuu 2025 tutakuwa na vituo vya afya katika kata zote.

“Ninaomba mnielewe, tunajenga kata zote saba za nje zinapata vituo vya afya kisha tunakuwa na hospitali ya wilaya na ya rufaa lengo ni kuhakikisha huduma za afya zinakuwepo,” alisema

Kuhusu changamoto, Aeshi alisema Sumbawanga umezungumzwa na vijiji 24, suala la umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) vinaingiziwa kwa zaidi ya laki tatu na si mitaa hivyo kumwomba Chongolo alifanyie kazi.

“Kuna vijiji hakuna umeme, mkandarasi anasumbua hivyo tunaomba uchukue hatua kwa kauli yako na maelekezo yako ili kuhakikisha wananchi wetu wanapata umeme wa uhakika na tunamskuru sana Rais Samia kwa kazi nzuri anayoifanya,” alisema.