Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila awaonya TRA kuhusu wanasiasa

Muktasari:

  • Amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wasikubali kukatishwa tamaa  kukusanya kodi na baadhi ya wanasiasa, ambao wamekuwa wakiwaeleza wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wasikubali kukatishwa tamaa  kukusanya kodi na baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiwaeleza wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, hivyo watakapowasumbua wapiga kura wao watapoteza kura zao.

Chalamila ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 17,2023 wakati wa mkutano na  watumishi wa TRA mkoani hapo, huku akisema siasa na utendaji haviendani hivyo watumishi hao wanatakiwa kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria.

"Nawatia moyo kazi yenu ya ukusanyaji wa mapato ina uhusiano mkubwa na siasa za nchi hii, hivyo msikubali kudanganywa na wanasiasa wakiwaeleza msiguse pale tunaelekea kwenye uchaguzi,’’amesema na kuongeza:

‘’ Nyinyi watumishi mnatakiwa mfanye kazi kwa mujibu wa sheria mtakapokusanya kodi itasaidia kuboresha barabara, hospitali, wanafunzi kupata fedha kwa ajili ya  mkopo wa elimu na watumishi kulipwa mishahara.

Pia amesema watumishi hao wafanye kazi kwa kufuata taratibu na kanuni walizojiwekea ikiwemo kujali utu, uadilifu mahali pa kazi na nje ya kazi, hivyo hatarajii kusikia mfanyakazi wa TRA akijihusisha katika vitendo viovu vya rushwa na utovu wa nidhamu.

Chalamila amesema Mkoa wa Dar es Salaam unategemewa kwenye makusanyo ya nchi kwa kuwa una mikoa mitano ya kikodi, una fursa ya kibiashara na una watu wengi walipa kodi  tofauti na mikoa mingine.

Aidha,  Chalamila amewataka watumishi hao kusimamia kwa juhudi na maarifa bila kuleta taharuki katika biashara, ukusanyaji kodi hasa kipindi cha Desemba mwaka huu, kwa kuwa ni msimu wa manunuzi makubwa na chanzo chake ni Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema watumishi hao  wasimamie matumizi sahihi ya mashine za kutolea risiti za kielekeroniki (EFD), ili kuhakikisha walipakodi wote wanatoa risiti sahihi za kodi na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali wanadai risiti.

Naye, Naibu Kamishna Kodi za ndani Divisheni ya Walipa Kodi Wadogo wa TRA, Edmund Kawamala amesema makusanyo  ya nchi,  yanategemea Mkoa wa Dar es Salaam ambao una mikoa ya kikodi mitano.

"Hakuna mkoa ambao una mikoa mingi ya kikodi kama Dar es Salaam, hivyo ukusanyaji wa kodi unatakiwa uwe wa maadili kwa kuwa ni nyenzo ya uwekezaji hadi vizazi vijavyo,’’ amesema.