Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila aunda timu kuchunguza uendeshwaji masoko Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika katika ofisi zake leo Jumamosi 19, 2023. Picha na Sunday George.

Dar es Salaam. Siku mbili tangu kuvunjwa kwa uongozi wa soko la Mababo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameunda kamati itakayofanya uchunguzi kwenye masoko yote.

Agosti 17 mwaka huu Mkuu huyo wa Mkoa alivunja unongozi wa soko hilo baada ya kupokea taarifa, akionyeshwa kukerwa na kitendo cha ubovu wa soko hilo, huku akiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi kuwasaka wahusika na kuwahoji waliofanya ubadhilifu wa fedha.

“Kuanzia sasa nimevunja uongozi wa soko uliokuwepo na Halmashauri na Mkurugenzi ndio watakusanya tozo katika soko hili na pia naagiza walifanyie maboresho madogo huku tukisubiri yale makubwa,”alisema Chalamila katika ziara yake.

Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi Agosti 19, 2023; Chalamila alisema kulikuwa na malamiko ya wafanyabiashara katika baadhi ya masoko, ambapo kuna watu wanaendesha masoko hayo kwa kujimilikisha kwa kubadili uongozi, na kuanza kuwapangishia na kuwauzia vyumba na maeneo ya kufanyia biashara.

Amesema masuala hayo wameshaanza kuyashughulikia, kwa kuanza na soko la mabibo ambalo kwa miaka zaidi ya mitatu limekuwa likikusanya mapato lakini hakuna fedha ambayo imewahi kwenda Serikalini.

 “Mapato ambayo yako pale sio chini y ash 900 milion lakini kuna kikundi kidogo cha watu kilichojiinua na kuanza kutishia uongozi, na kimekuwa kikila fedha hizo kwa muda mrefu tumechukua jukumu la kuvunja uongozi,” amesema Chalamila.

Alisema kufuatia ubadhilifu alioubaini kwenye baadhi ya masoko, ameamua kuunda timu itakayopita kwenye masoko yote, na kuangalia tija na mifumo inayotumika ili mwisho wa siku masoko yote yaweze kukarabatiwa.

 “Baada ya kuunda timu hii, itapita kwenye masoko yote na kuja na data kamili zitakazo husu mapato, mifumo inayotumika kukusanya mapato lakini pia na wanufaika,”amesema.

 “Timu hiyo ndani yake kuna watu kutoka Takukuru na haitafanya uchungiuzi tu bali itatushauri njia zipi zinazopaswa kutumika ili kukomesha upotevu wa mapato,”amesema Chalamila.

Akizungumzia suala la uhalifu katika jiji la Dar es Salaam Chalamila alisema, amebaini vipo vikundi vinavyojihususha na uhalifu hawatasita kuchukua sheria kwa mtu yoyote ambaye yuko tayari kuharibu amani ya mkoa huo.

Amesema endapo amani itaharibika mkoa wa Dar es Salaam, hakuna sehemu yoyote biashara itafanyika kwa amani, kwa kuwa ndio kitovu cha biashara, diplomasia na ndio eneo lenye watu wengi.

“Niendelee kuonya vikundi vyote vya kiasi, vinavyopanga au vilishapanga na kuratibu mbinu za kuharibu amani katika mkoa huu wajue kwamba tuna masikio yakutosha na tutawachukulia hatua kali, ili kuhakikisha tunadhibiti na kutojirudia tena kwa matendo kama hayo,” amesema.

Akizungumzia migogoro ya ardhi, amezionya kampuni, watu binafsi na wapimaji ambao wamekuwa ndio sehemu ya vichocheo ikiwa ni pamoja na utoaji wa hati zaidi ya moja.

Aidha Chalamila alisema, yapo maeneo yaliyo ya wazi lakini kumekuwepo na makundi ya watu wanaovamia na kuanza kuyapima bila ridhaa.

“Nitumie fursa hii kuonya wadau wa ardhi hapa kwetu wakiwemo watumishi, watu binafsi viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na wote wanaohusika katika mnyororo huo, na tumeshaanza kwa haraka kuanza kuishughulikia,”

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa tahadhari kwa wananchi, kutojihusisha na migomo isiyokuwa na tija na kuangalia athari zinazoweza kujitokeza.

Alieleza kuwa migomo sio njia yakusuluhisha matatizo hata kidogo, na kuwataka wananchi kutotishana kwa kuni viongozi wa mkoa huo hawatatetereka.

“Tumefungua milago ya mazungumzo lazima tukae na kuzungumza mara kwa mara ili angalau mambo yetu wote yaende kama yalivyotarajiwa,”amesema.