Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila ataka maduka Dar kutoa huduma saa 24, Kariakoo yatajwa

Muktasari:

  • Siku chache baada ya Serikali kuruhusu mabasi ya mikoani kusafiri saa 24, Mkoa wa Dar es umeahidi kuharakisha ya kufunguliwa kwa maduka saa 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema ataharakisha mpango wa maduka mkoani humo kutoa huduma saa 24 unatekelezwa. Hatua hii inakuja siku chache baada ya serikali kuruhusu mabasi ya mikoani kusafiri saa 24.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Julai 1, 2023 na Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila, kwenye bonanza la michezo kati ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na wafanyabiashara wa Kariakoo.

Maamuzi ya mabasi kusafiri saa 24 yalitolewa Juni 29 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiahirisha shughuli za Bunge jijini Dodoma.

Akizungumzia namna walivyojipanga, Chalamila amesema awali walikuwa wamejipanga kufanya biashara saa 24 baada ya kumalizika kwa ujenzi wa soko la Kariakoo Oktoba mwaka huu.
Lakini kutokana na maamuzi ya kuruhusu mabasi kusafiri saa 24, wanaona kuna haja ya kuharakisha mpango huo.

"Itakuwa ni aibu sana watu wanatoka mkoani usiku wanafika Dar na kutukuta tumefunga maduka, hivyo tutahakikisha tunaanza kufungua maduka saa 24 haraka iwezekanavyo na hivi karibuni tutaanza hata kwa majaribio kwanza," amesema Mkuu huyo wa mkoa.

Akizungumzia kuhusu bonanza hilo Chalamila aliwapongeza TRA kwa kulifanya kwa kile alichoeleza kuwa kinasaidia kuwaweka pamoja wafanyabiashara na TRA.

"Niwapongeze TRA kwa kuandaa bonanza hili kwani limewaleta pamoja na wateja wenu niwaombe andaeni na kwenye maeneo mengine mliyoyatenga kimkakati kwani itakuwa ni fursa pia ya kuoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi," amesema Chalamila.

Awali Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya TRA, Alphayo Kidata, amesema mashindano hayo yamehusisha tawi lao la mkoa wa kimkakati wa kikodi Kariakoo na watumishi wao wa TRA.

Kamishna Kidata ametaja michezo ambayo wameshindana kuwa ni pamoja na ķuvuta kamba, kufukuza kuku, mpira wa miguu na ule wa pete.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara, Martin Mbwana amesema bonanza hilo ni mwanzo mzuri wa uhusiano bora kutokana na yale waliyopitia hivi karibuni.

Mbwana ameahidi wataendelea kuhamasishana kulipa kodi bila shurti kwa kuwa sio jambo la mtu binafsi bali ni la nchi na ndizo zinazowezesha kuleta maendeleo katika nchi.