Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi wa JATU afikishwa kortini

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, baada ya kusomewa kesi ya kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (32) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.


Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.


Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi Desemba 29, 2022 na kusomewa shtaka lake na wakili wa Serikali Tumaini Mafuru, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio.


Akisomewa shtaka hilo, wakili Mafuru amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 207/2022 yenye shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili Mafuru amedai mshtakiwa andaiwa kutenda kosa hilo, katika ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika Jiji la Dar es Salaam, akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia Sh 5,139,865,733 kutoka Saccos ya JATU.


"Mshtakiwa wanadaiwa kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka Saccos ya JATU kwa kujipambanua kwamba fedha hiyo ataipanda kwenye kilimo na kuzalisha faida zaidi jambo ambalo alijua kuwa sio kweli" amedai wakili Mafuru.


Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake, alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.


Hakimu Mrio baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana kwa kesi yenye mashtaka au shtaka linalozidi kiwango cha Sh300 milioni.


Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 11, 2023 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.