Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi Jatu afikisha siku 369 akiwa rumande, bila upelelezi kukamilika

Muktasari:

  • Gasaya anakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo la kujipatia Sh5.1bilioni kwa njia ya udanganyifu, kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo cha mazao tofauti ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JATU  PLC, Peter Gasaya (33), anaendelea kusota rumande kwa kufikisha siku 369, kutokana upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili kutokukamilika.

Gasaya anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha kiasi hicho cha fedha.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai fedha hizo atazipanda kwenye kilimo cha mazao ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Mpaka leo, Januari 2, 2024, mshtakiwa huyo amefikisha siku 369, sawa na mwaka mmoja na siku 4 bila upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi dhidi ya kesi hiyo.

Kwa mara ya kwanza, Gusaya alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Desemba 29, 2022 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi.

Tangu siku hiyo hadi leo Jumanne, Januari 2, 2024 upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo kesi hiyo kuendelea kutajwa kila baada siku 14 mahakamani hapo.

Hata hivyo leo, Wakili wa Serikali, Erick Kamala ameieleza Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya kuwa Serikali bado inaendelea na upelelezi.

Kamala ametoa maelezo wakati kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutajwa.

Amedai licha ya upelelezi wa shauri hilo kutokukamilika, hakimu anayesikiliza shauri hilo Richard Kabate hayupo, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mbuya baada ya kusikiliza maelezo hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 15, 2024 itakapotajwa na mshtakiwa yupo rumande kutokana shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu ombi aliloomba mshtakiwa Desemba 18, 2023 la kutaka apatiwe mwenendo wa kesi hiyo ili waweze kuchukua hatua zaidi za kisheria, ombi hilo litatolewa uamuzi na hakimu anayesikiliza shauri hilo.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa, kati ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika jiji la Dar es Salaam, akiwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia Sh5.13 bilioni kutoka Saccos ya JATU.

Mshtakiwa wanadaiwa kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka Saccos ya JATU kwa kujipambanua kwamba fedha hiyo ataipanda kwenye kilimo cha mazao, jambo ambalo alijua kuwa sio kweli.

Shtaka la pili ni kutakatisha fedha tukio analodaiwa kulitenda kati ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika jiji la Dar es salaam.

Siku hiyo ya tukio na eneo hilo, mshtakiwa akiwa Mtendaji Mkuu na mwanzilishi wa JATU Saccos, alijihusisha na muamala wa Sh5.13 bilioni kutoka katika akaunti ya JATU Saccos iliyopo benki ya MNB tawi la Temeke kwenda katika akaunti ya JATU PLC liyopo katika benki ya NMB tawi la Temeke, wakati akijua fedha hizo zinatokana na kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mwisho.