Bodi ya Korosho yapokea dawa kuwanufaisha wakulima 40,000 Mtwara

Muktasari:

  • CBT imepokea lita 400,000 za dawa ya maji pamoja na salfa ya unga tani 10,000 katika msimu wa 2023/24 ambazo zitaanza kufanyiwa usajili pekee sambamba na mabomba 10,000.

Mtwara. Zaidi ya tani 49 za salfa ya unga pamoja na lita 3,100,000 za viuatilifu vya maji vinatarajiwa kupokelewa mkoani Mtwara kwaajili ya msimu wa 2023/24 huku lita 400,000 za maji pamoja na salfa ya unga tani 10,000 tayari zimeshawasili mkoani humo.

Akipokea pembejeo hizo Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred alisema kuwa viuatilifu hivyo vitagawiwa kwa wakulima waliosajiliwa pekee ambapo mpaka sasa zaidi ya wakulima 40,000 wakiwa tayari wamefikiwa na kusajliwa.

Alisema kuwa licha kuwahisha viwatilifu pia tunarajia kuwa na mabomba ya kupulizia 10,000 tumeanza kupokea viwatilifu hivyo ambapo tunaendelea kupokea pia tunayo mabomba ya kupulizia tutaendelea kupokea  na tunatarajia kupokea mabomba 10,000.

“Pamoja na kupokea viwatilifu tuona kuwa mkulima hana namna ya kupuliza hivyo tuliona umuhimu wa kupata mabomba ambapo tumeleta mabomba 10,000 ambapo tutayatoa wa wakulima ambao watalipia nusu bei kwa ruzuku,” amesema.

“Pia tunaendelea na usajili wa wakulima ambapo tutagawa kwa wakulima waliosajiliwa pekee ambapo mpaka sasa tumeshasajili zaidi ya wakulima 40,000 Mtwara, Nanyamba na sasa tuko Tandahimba,” amesema.

“Wakulima wajitokeze kujisajili na kutoa taarifa sahihi ambapo wasajili watahakikisha wanahesabu idadi ya mikorosho shambani picha na alama za vidole na kuchukua ukubwa wa shamba,” amesema.

“Tunatarajia kuanza kugawa katika maeneo ambayo yanawahi kupata korosho  uzalishaji tutaanza kusambaza mwezi wa nne ambapo ni vema wakulima wakapata namba maalum ili wasikose pembejeo hizo,” amesema.

“Serikali imetuwezesha kupata ruzuku ya serikali ambapo kwa sehemu kubwa viuatilifu hivi wamechangia yapo maeneo mengi yanaanza mwezi wa sita lakini maeneo yanayowahi tumetawahi pia kusambaza,” amesema.

“Tutaendelea kupokea sulfa kwa awamu na kuzigawa kwenda kwa wakulima jambo la kuwakumbusha wakulima ni wakulima hudumieni mashamba yenu Serikali ina nia dhamira kubwa kwenye zao hili tuunge mkono kwa kujitoa kwenye mashamba yetu na kuzingatia kanuni bora za kilimo cha korosho,” amesema.

“Pembejeo pekee haziwezi kukupa uzalishaji kama shamba haujalihudumia mfano sasa mvua zimeanza kunyesha mkulima makini tunaamini kuwa atakuwa tayari amesha palilia shamba lake ili maji yaweze kuingia ardhini najua wengi wameshakata matawi lakini kwenye kupalilia bado,” alisema Alfred.