Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bandari Mtwara kuzidi kufungua biashara Tanzania, Comoro

Balozi Tanzania nchini Comoro Pereira Ame Silima (wapili kushoto) akiongea jambo alipotembelea bandari ya Mtwara na ujumbe wa wafanyabiashara 20 kutoka katika kisiwa cha Ngazija nchini Comoro. Picha na Florence Sanawa

Mtwara, Ujumbe wa wafanyabishara 20 kutoka kisiwa cha Ngazija nchini Comoro umewasili mkoani Mtwara kwaajili ya kutafuta fursa mbalimbali za kibiashara.

Ugeni huo ulioongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Pereira Ame Silima pamoja na Balozi wa Comoro nchini Tanzania, Bacar Salim kutoka Kisiwa cha Ngazija ambapo wamefika mkoani hapa kwa lengo la kuangalia fursa za kibiashara.

“Awamu ya kwanza safari tulianza na watu wa kisiwa cha Muheli tena tukaleta wa Anjuani na sasa tumeleta wafanyabishara wa kisiwa cha Ngazija na matumaini ni makubwa kwakuwa wameshaanza kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka hapa nchini”

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas alisema kuwa wageni hao wamekuja kujionea fursa na wengi wamefurahishwa na utendaji wa bandari.

“Wapo walioomba meli ya moja kwa moja ili bidhaa zikitoka Mtwara ziende moja kwa moja walipo katika kisiwa cha Ngazija ili kupunguza bidhaa kuharibika kutokana na kusafiri kwa muda mrefu barabarani”

“Kwa sasa hili jambo tutalifanyia kazi hii ni fursa kubwa wengi wamesema wanatamani tutatue changamoto hiyo ni wajibu wetu kuwaunganisha Mtwara na wakazi wa Comoro na tulishaanza mazungumzo na kampuni zenye meli ambayo ilishaahidi kuja kutoa huduma” alisema Kanal Abbas

Mwakilishi wa Meneja wa bandari mkoa wa Mtwara, James Ngw’andu alisema kuwa mpaka sasa shehena ya kwenda nchini Comoro imekuwa ikiongezeka kutokana na wafanyabishara kufika nchini na kuona fursa wanazoweza kuzifanya.

“Kuna wakati tulihudumia tani 15,760  lakini kwa miezi sita kuanzia Julai-Desemba tuliweza kusafirisha tani 9,585 ambapo shehena inayosafirishwa kwenda Comoro imekuwa ikiongezeka ambapo tunasafirisha saruji mwaka jana ilichukua asilimia 97 ya shehena kwa miezi 6 asilimia 86 lakini kuna juisi chakula na vifaa vya ujenzi”

“Katika kipindi hicho zaidi ya meli 17 meli nazo zinazohudumia meli 18 kwenda Comoro lakini kwa kipindi cha miezi sita tuliweza kuhudumia meli 17 utaona kiasi ambacho zinaongezeka”

“Changamoto kubwa ni ukosefu wa uhakika wa meli ya kusafirisha shehena kutoka Mtwara kwenda Comoro na Zanzibar ambapo inafanyiwa kazi ili kuweza kuitatua” alisema Ngw’andu

Shemsia Said ambaye ni mfanyabishara kutoka nchini Comoro alisema kuwa tunaweza kufanyakazi pamoja kwa kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka huku na kuja kwetu kwakuwa tuna uhitaji mkubwa zaidi.

“Tunataka chakula na mavazi ndio maana tunapita na kuangalia nini tunaweza kununua ama kuleta nataka kujua kama naweza kuleta bidhaa zangu katika nchi hii na nikaziuza ndio maana ya ujio huu”