Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bajeti ya Serikali yapitishwa

Muktasari:

  • Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023 ya Sh41.48 trilioni imepitishwa na wabunge leo Ijumaa, Juni 24,2022 baada ya wabunge 356 kati ya 379 kupiga kura za ndio.

Dodoma. Bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023 ya Sh41.48 trilioni imepitishwa na wabunge leo Ijumaa, Juni 24,2022 baada ya wabunge 356 kati ya 379 kupiga kura za ndio.

Akitangaza matokeo bungeni leo Ijumaa Juni 24,2022 Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema jumla ya wabunge 379 waliokuwepo bungeni walipiga kura.

Amesema hakuna mbunge aliyesema hapana huku wabunge 23 wakisema hawana maamuzi.

Waliopiga kura za sina maamuzi ni pamoja na wabunge wa viti maalum waliofukuzwa uanachama na Chadema.