Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bahati Nasibu ya Taifa sasa kidijitali kupitia Vodacom

Dar es Salaam. Katika hatua ya kuboresha huduma na kuongeza ushiriki wa wananchi katika michezo ya bahati nasibu, Bahati Nasibu ya Taifa imetangaza ushirikiano rasmi na Vodacom M-Pesa. Ushirikiano huu unalenga kurahisisha miamala ya kidijitali kwa wachezaji wa bahati nasibu na kupanua fursa za kibiashara kupitia mfumo wa fedha wa simu. 

Kwa makubaliano haya, watumiaji wa Vodacom M-Pesa sasa wataweza kununua tiketi za michezo ya bahati nasibu kwa njia ya simu, wakitumia USSD, aplikesheni ya M-Pesa au njia zingine za malipo zinazopatikana kwenye jukwaa la Vodacom. 

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania, Kelvin Koka, amesema kuwa ushirikiano huu utarahisisha upatikanaji wa huduma za bahati nasibu kwa Watanzania wengi zaidi, huku ukihakikisha usalama na uwazi wa miamala. 

"Kwa kushirikiana na Vodacom M-Pesa, tunahakikisha kuwa wachezaji wanapata huduma kwa urahisi na haraka kupitia jukwaa salama na la kuaminika. Ushirikiano huu pia unaleta fursa kwa wafanyabiashara kushirikiana nasi katika sekta hii inayoendelea kukua kwa kasi," amesema Koka. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya M-Pesa Tanzania, Jacqueline Ikwabe, ameeleza kuwa Vodacom inaendelea kuboresha mifumo yake ili kuwahakikishia wateja huduma bora zaidi za kifedha kwa njia ya simu. 

"M-Pesa imejikita katika uvumbuzi wa kidijitali unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania kwa kutoa suluhisho rahisi na salama. Kwa kuiunganisha Bahati Nasibu ya Taifa kwenye mfumo wetu, tunawapa wachezaji njia nyepesi ya kushiriki na kuongeza ufanisi katika huduma za michezo ya bahati nasibu," amesema Ikwabe. 


 Fursa zaidi kwa wananchi 

Bahati Nasibu ya Taifa inatarajia kutumia ushirikiano huu kama njia ya kuongeza uelewa wa huduma zake kabla ya uzinduzi rasmi. Hatua hii itawezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki kwa urahisi na kwa usalama, huku ikiongeza fursa za ushiriki kwa makundi mbalimbali ya watu. 

Ujumuishwaji wa jukwaa la Bahati Nasibu ya Taifa kwenye mfumo wa Vodacom Tanzania pia unatarajiwa kusaidia kupanua wigo wa huduma za michezo ya bahati nasibu, kuongeza mapato ya sekta, na kusaidia ukuaji wa uchumi kupitia mfumo wa kidijitali.