Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Babu wa Loliondo afariki dunia

Arusha. Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kwa jina la 'Babu wa Loliondo', ambaye alipata umaarufu wa kutoa tiba ya kikombe kilichokuwa kinadaiwa kutibu magonjwa mbalimbali amefariki dunia.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa mzee huyo, Paul Dudui zimesema mzee Mwasapile amefariki leo Ijumaa Julai 30, 2021 mchana katika kituo Cha Afya Cha Digodigo baada ya kuugua ghafla.

"Nikweli mzee amefariki muda huu ndio tunasubiri mwili uletwe hapa chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya Wasso" amesema Dudui

Dudui amesema mwili huo utapokelewa na viongozi wa Serikali wa Wilaya ambao ndio watatoa taarifa rasmi.

"Huu msiba mkubwa kwa wilaya nzima ya Ngorongoro na Kata ya Samunge alipokuwa anaishi mzee kwani ameleta mafanikio makubwa kutokana na kikombe cha dawa alichokuwa anato "amesema

Amesema kabla ya kifo aliugua wiki iliyopita na kupewa matibabu kurejea nyumbani na leo ndio hali ilibadilika ghafla na kukimbizwa kituo cha Afya cha Digodigo na kufariki.

Taarifa zaidi kukujia……