Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba adaiwa kumnyonga mwanaye kwa waya

Muktasari:

  • Baba amuua mtoto wake kisha akujipiga picha kwa kutumia simu yake huku mwili wa marehemu huyo ukiwa umeuning'inizwa katika mlango wa chumba ambacho wanalala, huku akicha ujumbe wa maandishi akidai kuwa kulikuwa na mgogoro kati yake na mke.

Iringa. Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linamsaka Goodluck Mgovano kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake mwenye umri wa miaka (2).

 Inadaiwa kuwa baada ya kitendo hicho, baba huyo alikimbia na mpaka sasa bado hajulikani alipo japo juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Akizungumnza kwa njia ya simu na Mwananchi Digital leo Jumamosi 28, 2023; Kamanda Polisi mkoani Iringa, Allan Bukumbi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea Oktoba 27, mwaka huu, saa 1: 20 usiku, katika eneo la Mlandege, Manispaa ya Iringa.

Aidha Kamanda Bukumbi amejata jina la mtoto huyo kuwa Alvin Goodluck Mgovano ambaye anadaiwa kufariki baada ya kunyongwa na baba yake mzazi kwa kutumia waya.

Kamanda huyo ameeleza kuwa kabla ya tukio hilo, saa 10:00 jioni, mtuhumiwa huyo alienda kumchukua mtoto huyo mtaa wa Mlandege katika moja ya mashine za kukoboa mpunga maarufu mashine ya Ngwale ambako mtoto huyo alikuwa na mama yake Milliam Abasi ambaye ni mke wa Mtuhumiwa.

"Mtuhumiwa alimchukua mtoto kutoka kwa mama yake na kuondoka naye kwenda nyumbani na kisha  kumnyonga na kumning'iniza katika mlango wa chumba ambacho wanalala kisha akajipiga picha kwa kutumia simu yake akiwa na mwili wa marehemu huyo.

Kamanda Bukumbi amesema kuwa baada ya tukio hilo, mtuhumiwa aliacha ujumbe wa maandishi akidai kuwa walikuwa na mgogoro kati yake na mke hivyo anaomba mtoto wake akazikwe katika Kijiji cha Utengule.

"Baada ya kuacha ujumbe huo uliodai alikuwa na mgogoro kati yake na mke wake kutokana na tukio ambalo lilitokea Oktoba 6 ambalo  bado halijafahamika ni tukio gani analodai alifanyiwa na mke wake huyo," alieleza kamanda huyo

Kamanda Bukumbi ameongeza kuwa yapo matatizo ambayo yanatokea kwenye familia na hivyo kusababisha watu kuwa na changamoto za msongo wa mawazo.

“Tukio kama hili la kumnyonga mtoto ni kumpa adhabu kubwa ambayo hakustahili hivyo ni muhimu wananchi kutafuta namna ya kutatua matatizo yao ya kifamilia ikiwa ni pamoja na kupata ushauri kwa wasaikolojia ili kuepukana na matukio hayo," amesema

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani hapa bado linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.