Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanafunzi chuo kikuu amnyonga mwenzake

Mwanafunzi chuo kikuu amnyonga mwenzake

Muktasari:

  • Amesema baada ya wazazi kupata taarifa hizo waliripoti kituo cha polisi, ndipo askari walikwenda katika nyumba ya mtuhumiwa na kuukuta mwili wa marehemu.

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Iringa, Petronel Mwanisawa (22) amefariki dunia kwa kunyongwa na mpenzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mtuhumiwa, Prudence Patrick (21), ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda Bwire amesema tukio hilo limetokea Juni 1, mwaka huu maeneo ya Kihesa.

Amesema siku ya tukio marehemu hakurudi nyumbani kwao jambo ambalo si kawaida yake, hivyo wazazi wake waliingiwa na hofu na kuanza kumtafuta.

"Marehemu alikuwa anaishi na wazazi wake, na huyu mtuhumiwa yeye alikuwa amepanga. Kwa hiyo siku ya tukio alitoka kwenda chuo, lakini mpaka usiku akawa hajarudi, ndipo wazazi walianza kupata wasiwasi, wakampigia simu rafiki yake lakini hawakufanikiwa," amesema Kamanda Bwire na kuongeza:


"Kwa hiyo jana ndo tukampata, na hiyo ni baada ya mtuhumiwa mwenyewe kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa mzazi wa marehemu akisema alikuwa na Petronel na kwamba amefariki. Baada ya hapo hakupatikana tena," alisema.

Amesema baada ya wazazi kupata taarifa hizo waliripoti kituo cha polisi, ndipo askari walikwenda katika nyumba ya mtuhumiwa na kuukuta mwili wa marehemu.

Bwire amefafanua kuwa, taarifa za awali zinaonyesha binti huyo alinyonyongwa na mpenzi wake na chanzo ni wivu wa mapenzi.

"Mtuhumiwa tulimkamata njia ya kuelekea Dodoma alipokuwa akijaribu kutoroka na upelelezi wa tukio hilo unaendelea," amesema Kamanda Bwire.