Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya ushindi, Ngorongoro kuboresha miundombinu

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Abdul-razaq Badru, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha leo Jumatatu Juni 30,2025 baada ya mamlaka hiyo kushinda tuzo ya kuwa kivutio bora barani Afrika iliyotolewa na  mtandao wa World Travel Awards (WTA).

Muktasari:

  • Hii ni mara ya pili Ngorongoro kushinda tuzo hiyo ya kivutio bora barani Afrika mwaka 2025 (Africa’s Leading Tourist Attraction 2025) inayotolewa na mtandao wa World Travel Awards (WTA), ambapo kwa mara ya kwanza ilishinda tuzo hiyo Oktoba 15, 2023.

Arusha. Baada ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kushinda tuzo ya kivutio bora cha utalii barani Afrika mwaka 2025 iliyotolewa na mtandao wa World Travels Awards (WTA), Mamlaka hiyo imeandaa mkakati wa kuboresha miundombinu yake ikiwemo ya barabara ivutie watalii zaidi na kuongeza bidhaa mpya za utalii.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 30, 2025 na Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Abdul-razaq Badru, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa hafla ya kuwavalisha vyeo na kuwaapisha makamishna wasaidizi waandamizi wa uhifadhi na makamishna wasaidizi wa uhifadhi.

Hii ni mara ya pili NCAA kushinda tuzo hiyo barani Afrika, ambapo mara ya kwanza ilishinda Oktoba 15, 2023.

Amesema tuzo hiyo inawapa nguvu ya kusonga mbele kwa kasi na kuwa wamedhamiria kuboresha miundombinu yake yote ikiwemo ya barabara, vituo vya ulinzi na usaidizi, vituo vya watoa taarifa na malazi ya watalii.

 “Moja ya vipaumbele vyetu ni kuboresha miundombinu yetu iweze kufanya vizuri na kuvutia watalii zaidi, tunakamilisha muundo mpya wa malipo na wadau watafanya malipo popote wakiwa duniani hawatapita mfumo mwingine,” amesema.

Kamishna huyo amesema mbali na maboresho hayo wanatarajia kuzindua bidhaa mpya ya utalii ambayo itaingia sokoni hivi karibuni na itatoa fursa kwa wadau wengi wa masuala ya utalii kujifunza, lengo likiwa ni kuhakikisha chapa ya NCAA inakuwa juu na kuaminika zaidi.

“Tunatarajia maboresho na bidhaa mpya ya utalii itaongeza watalii na dhamira yetu katika kipindi cha miaka miwili au mitatu, idadi ya watalii iwe maradufu ili ichangie maendeleo ya kiuchumi na kijamii na jamii zinazozunguka eneo lile zitanufaika pia,” amesema.

Awali akizungumza katika hafla hiyo wameapishwa makamishna saba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana amesema anataka walioapishwa kuhakikisha wanafanya kazi wakitanguliza nidhamu, maadili, bidii na kulinda uhifadhi.

Amewataka kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi rasilimali za Ngorongoro pamoja na kutangaza vivutio vilivyopo katika mamlaka hiyo.

“Mnapovaa vyeo vya kijeshi mnapaswa kuonyesha dhamira ya dhati, kutumikia na kulinda eneo la NCAA na kuelewa vyeo hivi vinakuja na majukumu makubwa ambayo yanahitaji mjitume na kuwajibika.

 “Uongozi bora hauji kwa bahati unahitaji maandalizi, mafunzo na dhamira ya kweli kujifunza na kubadilika, mfumo wa jeshi usu ni muhimu sana kuanzia chini mpaka juu kwani huwezi kuongoza watu wenye taaluma fulani ambayo wewe huna, utayumbishwa kila wakati na taasisi haitaweza kuwa imara,” amesema.

“Bodi itaendelea kushirikiana na Menejimenti ya NCAA ili iwe na uongozi thabiti, maadili, weledi na maono ya muda mrefu. Msisahau leo mmebeba matumaini mapya ya taasisi, tuonyeshe dunia kuwa NCAA ina watu sahihi,” amesema.