Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aweso ataja mikakati ya kufikia vipaumbele

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza bungeni Jumanne Mei 5, 2026 wakati akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake.

Muktasari:

  • Mikakati hiyo ni kuimarisha suala la rasilimali watu akisema watatumia weledi wa watumishi na kuwajengea uwezo wa kutekeleza vipaumbele vya wizara, ushirikishwaji wa sekta binafsi na kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Maji.

Dodoma. Wizara ya Maji imetaja mikakati sita itakayosaidia kuvifikia vipaumbele saba kwenye sekta ya maji kwa mwaka 2026/27.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 5, 2026 wakati akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake ambapo amesema wizara mikakati hiyo itasaidia kufikia malengo ya misingi pamoja na vipaumbele saba katika wizara.

Mikakati hiyo ni kuimarisha suala la rasilimali watu akisema watatumia weledi wa watumishi na kuwajengea uwezo wa kutekeleza vipaumbele vya wizara, ushirikishwaji wa sekta binafsi na kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Maji.

“Tutaimarisha upatikanaji wa vyanzo mbadala vya fedha ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji na kupunguza utegemezi kwa Serikali, kama bodaboda moja mjini Pangani ilivyoandikwa bila nyenzo Hutoboi,” amesema Aweso.

Waziri amesema mpango huo ni endelevu na wa ubunifu wa kifedha utakaoiwezesha sekta ya maji kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa kasi na uhakika kwa kuwa Dira 2050 inaelekeza asilimia 70 ya fedha za uwekezaji kuchangiwa na sekta binafsi.

Amesema wizara imeanza kutekeleza maelekezo hayo, kwa kuimarisha ushirikiano na washirika wa maendeleo, taasisi zisizo za kiserikali na sekta binafsi kwa ajili ya kupata vyanzo mbadala vya fedha vitakavyotumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye Sekta ya Maji ili kupunguza utegemezi kwa Serikali.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza bungeni leo Jumanne Mei 5, 2026 wakati akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake.

Kwenye kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Maji, amesema wizara itaendelea kuuimarisha mfuko huo ili kuongeza uwezo wake wa kupata fedha za kugharamia miradi 27 ya maji, kuendeleza vyanzo vya maji na kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma ya maji.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza bungeni leo Jumanne Mei 5, 2026 wakati akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake.

Amesisitiza suala la matumizi ya Tehama ili kuboresha utoaji wa huduma kupitia teknolojia za kisasa ambapo mifumo mbalimbali inaboreshwa, ikiwemo mifumo ya kusoma mita kidijitali na maombi ya maunganisho ya maji kidijitali.