Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aweso aamuru wasaidizi wake wabaki Songwe

Waziri wa Maji,  Jumaa Aweso.

Muktasari:

  • Waziri wa maji aamuru baadhi ya wasaidizi wake kubaki Wilaya ya Songwe kuanzisha mchakato wa uanzishaji mamlaka ya maji.

Songwe. Waziri wa Maji,  Jumaa Aweso ameagiza watendaji wa Wizara yake kuunda mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Mkwajuni ili kurahisisha utendaji na kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Aweso amesema hayo leo Julai 31, mwaka huu katika siku yake ya kwanza ya ziara ya siku mbili Mkoani hapa baada ya kupokea taarifa kuwa kata za Mkwajuni na Saza zina idadi kubwa ya watu, hivyo kuhitaji msukumo wa karibu wa usimamizi na upatikanaji wa maji.

Amesema kwa kuanza kuunda mamlaka hiyo Mkurugenzi Idara ya Isambazaji maji Vijijini kutoka wizarani Joyce Msiro na Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Ruwasa makao makuu, Mhandisi Mengo Ndele wakisaidiana na viongozi wengine wa mkoa wabaki wilayani Songwe ili kuanzisha mchakato na kuwa ndani ya mwezi huu Wizara itapeleka Sh500 milioni ili kuanzisha mamlaka hiyo ikiwemo na shughuli zingine.
"Hii ni awamu yangu ya pili kuja Wilaya ya Songwe nimeona mabadiliko makubwa mji umechangamka na naona pilikapilika za biashara ni nyingi, kwa hali hiyo uhitaji wa mamlaka ya maji ni mkubwa," amesema Aweso.

Aidha amesema wizara yake imefanya kazi kubwa ya kuweka miundombinu ya maji wilayani humo ambapo kati ya vijiji 43 vilivyopo, vijiji 41 tayari vimewekewa miundombinu hiyo.
Aweso amemuagiza Meneja wa Ruwasa Mkoa Songwe, Mhandisi Charles Pande kutafuta Sh500 milioni kutoka fungu la uendeshaji ili kununua magari matatu ambayo moja lipelekwe wilayani Songwe kwa ajili ya usimamizi.
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo, Solomon Itunda akiwasilisha taarifa ya wilaya amesema halmashauri ya wilaya hiyo imetenga zaidi ya Sh526 milioni na hivyo kuwa na upungufu wa Sh1.5 bilioni Ili kuimarisha upatikanaji wa maji katika kata za Mkwajuni na Saza.

 Mbunge wa Songwe, Philpo Mulugo alimwambia Waziri Aweso kuwa utendaji wake umesaidia wilaya yake kupata miradi mingi ya maji na hivyo kupunguza kero ya ukosefu wa maji ilivyokuwa inawakabili wananchi ambao walikuwa wakipata maji ya  visima ambayo pia yana harufu ya magadi.