Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa maji Shinyanga watakiwa kukamilika Agosti

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akiwa na Mbunge wa Solwa Ahmes Salum wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Mwalukwa wilayani Shinyanga katika ziara ya kukagua miradi ya maji. Picha na Suzy Butondo

Muktasari:

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Cyprian Luhemeja ameiagiza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shuwasa), kuhakikisha mkandarasi anatekeleza kazi ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa vijiji 22 katika mradi wa maji Tinde wilayani Shinyanga kufikia Agosti mwaka huu.

Shinyanga. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Cyprian Luhemeja ameiagiza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (Shuwasa), kuhakikisha mkandarasi anatekeleza kazi ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa vijiji 22 katika mradi wa maji Tinde wilayani Shinyanga kufikia Agosti mwaka huu.

Agizo hilo amelitoa wakati alipotembelea mradi huo katika tanki la kuhifadhia Maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria lenye lita za ujazo 1.1 milioni lililopo kijiji cha Buchama Kata ya Tinde wilayani Shinyanga ambalo linatarajiwa kunufaisha wananchi 20,201.

Amesema mradi huo umeshakamilika kwa asilimia kubwa na tayari fedha za kusambaza huduma ya maji kwa wananchi zipo.

“Mkurugenzi nakuagiza wasiliana na meneja mradi ili mkandarasi ambaye anafanya kazi hii ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi hadi kufikia mwezi Agosti awe ameshaanza kazi mara moja na kuvifikia vijiji vyote 22,”amesema Luhemeja

Akiwa katika Kata ya Mwalukwa kukagua utekelezaji wa miradi ya maji, aliziagiza pia mamlaka za maji zote kutoa elimu kwa wananchi kuvuta mabomba ya maji majumbani mwao, ili kutekeleza adhima ya kumtua ndoo kichwani mwanamke na kuacha kuchota maji kwenye vituo.

Kaimu Mkurugenzi wa Shuwasa, Sarah Emmanuel amesema mkandarasi ambaye amejenga tanki hilo la maji ndiyo ambaye atatekeleza kazi ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi.

"Mamlaka inatekeleza mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba za usambazaji takribani kilomita 8.1 kwa awamu ya kwanza utakaohudumia vijiji vya Jomu na Nyambui ambao umegharimu zaidi ya Sh24 bilioni,” amesema

Amesema kwa mradi wa Tinde pekee umegharimu Sh5 bilioni na utekelezaji wake ulianza Agosti 2021 ukiwa umesanifiwa kuwahudumia wananchi 60,000.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata huduma ya majisafi na salama ya Ziwa Victoria, akiwemo Anna Tungu amesema mradi huo umewaondolea adha ya maji kutembea kilometa 10 kufuata huduma hiyo.

Naye Diwani wa Tinde Jafari Kanolo, amesema katika mradi huo licha ya kijiji cha Buchama ambapo mradi huo upo hawajapata maji hivyo kuomba maeneo yote yapatiwe maji.

Mbunge wa Solwa wilayani Shinyanga, Ahmed Salum ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha na kutekelezwa miradi ya maji safi na salama jimboni mwake akidai kwa sasa asilimia kubwa ya wnaanchi hawana changamoto ya huduma hiyo nakuwa vijiji vichache ambavyo havina maji vitafikishiwa.