Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Gwajima awasili bungeni kuendelea kuhojiwa

Askofu Gwajima awasili bungeni kuendelea kuhojiwa

Muktasari:

  • Mbunge wa Kawe (CCM),   Askofu Josephat Gwajima amewasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Dodoma. Mbunge wa Kawe (CCM),   Askofu Josephat Gwajima amewasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Gwajima alihojiwa mara kwanza na kamati hiyo Agosti 23, 2021 ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo,  Emmanuel Mwakasaka amesema kuwa mahojiano bado yanaendelea.

Mbunge huyo amefika bungeni katika viwanja vya Bunge saa 6:20 mchana na kwenda katika kikao cha kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambapo yeye ni mjumbe.

Baadaye akiwa ameongozana na askari alishuka na kuketi katika viti vilivyo karibu na mashine ya kukaguliwa ya jengo la utawala la Bunge.