Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Dk Mutungi afariki dunia

Muktasari:

  • Ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa kwanza tangu kuasisiwa kwa chama hicho.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kifo cha aliyekuwa kada wake, Dk Medard Mutungi, aliyefariki dunia leo, Aprili 2026 jijini Dar es Salaam.

Dk Mutungi, aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara kuanzia mwaka 1998 hadi 2004, akiwa miongoni mwa viongozi wa mwanzo enzi za kuasisiwa kwa chama hicho.

Taarifa ya kifo chake, imetolewa leo, Jumapili Aprili 26, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia.

"Chama kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Bara, Dk Medard Mutungi, kilichotokea leo tarehe 26 Aprili 2026 mkoani Dar es Salaam," imesema taarifa hiyo

Chama hicho kupitia taarifa hiyo, kimetoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na wanachama wote kwa msiba huu mzito.

"Tunawaombea wafiwa wote kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu," imeeleza taarifa hiyo.

Imesema chama hicho kitaendelea kushirikiana na familia katika kipindi chote cha maombolezo na kitatoa taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana.