Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyeingia Tanzania bila kibali, atozwa faini ya Sh1 milioni

Mshtakiwa Devanshu Dusad (kulia) akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu, akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa mashtaka ya kuingia nchini bila kuwa na kibali pamoja na kufanya biashara bila kuwa na kibali. Picha Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Dusad amehukumiwa kifungo hicho, leo Jumanne Novemba 19, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukiri mashtaka yake mawili na Mahakama kumtia hatiani


Dar es Salaam. Raia wa India, Devanshu Dusad (24) amehukumiwa kulipa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kupatikana na makosa mawili ikiwamo kuishi nchini Tanzania bila kibali.

Dusad amehukumiwa kifungo hicho, leo Jumanne Novemba 19, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukiri mashtaka yake mawili na Mahakama kumtia hatiani.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa faini hiyo na kukwepa kifungo.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, mshtakiwa huyo, alijitetea kuwa anaomba apunguziwe adhabu kwa sababu viza yake iliisha Oktoba na alikuwa katika utaratibu wa kutengeneza nyingine.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, amesema mshtakiwa ametiwa hatiani kama alivyoshtakiwa.

"Kutokana na mshtakiwa kukiri shtaka lake mwenyewe bila kulazimishwa, Mahakama imezingatia upande wa mashtaka hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma dhidi ya mshtakiwa, hivyo ina kuhukumu kulipa faini ya Sh 500,000 kwa kila shtaka au kwenda gerezani miezi 12 kwa kila kosa," amesema Hakimu.

Awali, wakili kutoka Idara ya Uhamiaji, Ezekiel Kibona aliiomba Mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria ili iwe funzo kwa raia wa kigeni kuishi nchini bila kufuata utaratibu.

Akimsomea hati ya mashtaka, Wakili Kibona alidai kuwa, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 13, 2024 katika ofisi za Commododities Tanzania Ltd zilizopo Mtaa wa Samora, jijini hapa.

Alidai siku hiyo ya tukio, mshtakiwa akiwa raia wa India alikutwa akiishi nchini bila kuwa na nyaraka yoyote inayoonesha  ni raia wa India huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. 

Shtaka la pili, siku na eneo hilo akiwa raia wa India, alikutwa akifanya biashara, bila kuwa na kibali cha kazi.

Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka na hoja za awali (PH)alikiri kutenda kosa hilo na ndipo Mahakama ilimtia hatiani na kumhukumu