Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyeishi Tanzania bila kibali kwa kumpenda Magufuli ahukumiwa kulipa faini ya Sh1.2 milioni

Aliyeishi nchini bila kibali kwa kumpenda JPM ahukumiwa kulipa faini ya Sh1.2 milioni

Muktasari:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu raia wa Uganda, Noah Mukobe, kulipa faini ya Sh 1.2milioni au kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini bila kuwa na kibali.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu raia wa Uganda, Noah Mukobe, kulipa faini ya Sh 1.2milioni au kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini bila kuwa na kibali.

Mshtakiwa huyo alidai kuwa ameingia nchini kwa sababu anaipenda Tanzania na anampenda Rais John Magufuli kwa sababu ameukomesha ugonjwa wa Cov-19, nchini mwake.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, baada ya mshtakiwa huyo kukiri mashtaka yake wakati akisomewa mashtaka.

“Mshtakiwa ametiwa hatiani hivyo Mahakama hii inamhukumu kulipa faini na kama atashindwa kulipa faini basi atatumikia kifungo” alisema.

Hakimu Shaidi alisema katika shtaka la kuingia nchini bila kuwa na kibali, mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh 600,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Shtaka la pili, ambalo ni kuishi nchini bila kufuata utaratibu, Mukobe anatakiwa kulipa faini ya Sh 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja jela. Hata hivyo, Mukobe alifanikiwa kulipa faini hiyo na kuepuka kifungo.

Awali, Wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo alidai, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda makosa yake, Novemba 24, 2020 eneo la Ubungo.

Wakili Ngwijo alidai siku hiyo ya tukio, mshtakiwa aliingia nchini bila kuwa na kibali na baada ya hapo aliishi nchini bila kufuata utaratibu, kwa maana ya kutokuwa na kibali cha kuishi nchini, wakati akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake alikiri kuingia na kuishi nchini bila kuwa na kibali, hali iliyosababisha mahakama kumtia hatiani na kumhukumu kulipa faini.

Kabla ya mahakama kutoa hukumu hiyo, Hakimu Shaidi alimuuliza mshtakiwa kama ana lolote la kusema.

Mshtakiwa alijibu analo la kuzungumza na alipopewa nafasi alianza kujitetea sababu ya yeye kuingia nchini bila kuwa na kibali.

Mshtakiwa alidai kuwa aliiingia nchini kwa sababu anaipenda Tanzania na anampenda Rais John Magufuli kwa sababu kaukomesha ugonjwa wa Cov-19.

“Mheshimiwa hakimu, nimekiri kuwa nimeingia Tanzania kimakosa kwa sababu naipenda Tanzania na kuna ndugu zangu wako hapa na nampenda Rais John Pombe Magufuli kwa sababu kaikomesha corona, hivyo naomba nipunguziwe adhabu” alidai mshtakiwa.

Mshtakiwa baada ya kujitetea hivyo, wakili Ngwijo aliiomba mahakama itoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo kwa sababu alikuwa anajua taratibu za kufuata ili aweze kuingia nchini.

“Mshtakiwa ni muelewa na mkosaji kwa mara ya kwanza, hivyo kama alijua kuna taratibu za kufanya ili aweze kuvuka mipaka na alikuwa na hati ya kusafiria, lakini kwa makusudi akaamua asifanye hivyo, naiomba Mahakama impe adhabu kali,’’ alisema Wakili Ngwijo.