Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT- Wazalendo yasisitiza miswada izingatie maoni ya wadau

Naibu Katibu Mwenezi, Habari na Mahusiano na Umma wa ACT-Wazalendo, Janeth Rithe

Muktasari:

ACT-Wazalendo imewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Tanga, chama hicho kitaendelea kusukuma uboreshaji wa miswada hiyo ili nchi iweze kuwa na uhuru wa kisiasa kama Taifa

Dar es Salaam. ACT- Wazalendo imeendelea kuisisitiza Serikali kuhakikisha miswada mitatu ya sheria za uchaguzi iliyopelekwa bungeni kuboreshwa inaakisi maoni na mapendekezo ya wadau wa demokrasia nchini.

Miswada hiyo iliyowasilishwa bungeni Novemba 10, 2023 ni Muswada wa Tume ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, Muswada wa Sheria wa Vyama vya Siasa na Muswada wa Gharama za Uchaguzi.

Kauli hiyo ya ACT- Wazalendo inakuja ikiwa tayari makundi mbalimbali yameshawasilisha maoni yao kwa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitangaza kufanya maandamano kushinikiza miswada hiyo kuondolewa bungeni.

Chadema imetangaza uamuzi huo leo Jumamosi, Januari 13, 2024 kupitia kwa mwenyekiti wake, Freeman Mbowe alisema maandamano hayo yatafanyika Januari 24, 2024.

Wakati Mbowe akitoa msimamo huo, taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Naibu Katibu Mwenezi, Habari na Mahusiano na Umma wa ACT-Wazalendo, Janeth Rithe imeeleza msimamo huo wa chama umetolewa kwa nyakati tofauti kupitia hotuba ya Makamu Mwenyekiti (Bara) Doroth Semu na Naibu Katibu Mkuu-bara, Joran Bashange.

Katika taarifa hiyo imeeleza viongozi hao wa ACT-Wazalendo imewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Tanga, chama hicho kitaendelea kusukuma uboreshaji wa miswada hiyo ili nchi iweze kuwa na uhuru wa kisiasa kama Taifa pamoja na kuhakikisha chaguzi zote zijazo zinakuwa huru, haki na zinazoaminika.

Semu pia alisisitiza chaguzi zote zikiwamo za Serikali za mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni lazima zisimamiwe na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huku akipinga kifungu cha sheria kinachowaruhusu wakurugenzi wa halmashauri na majiji kusimamia chaguzi za aina zote.

 “Kupitia miswada hiyo, sheria iweke kifungu mahususi cha kuzuia mtu ambaye amewahi kushiriki kwenye siasa asiwe msimamizi wa uchaguzi.

“ACT Wazalendo inapendekeza kuwepo kifungu cha sheria kinachoruhusu wajumbe wawili kwenye Tume ya Uchaguzi wanaotokana na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kwa kuzingatia jinsia huku pia ikitaka sheria ya vyama vya siasa iwe na kifungu cha kuvibana na kuvielekeza vyama vyote kwenye nafasi za uamuzi kuwepo wanawake kwa kiwango fulani,” imeeleza taarifa hiyo

Pia, ACTI Wazalendo inapendekeza kuwapo kwa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa kulingana na mapendekezo ya kikosi kazi ili kusaidia kujiendesha na kuepuka matumizi ya fedha chafu.