Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT Wazalendo walaani shambulio Padri Kitima

Muktasari:

  • Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inaendelea na uchunguzi wa shambulio la kiongozi wa dini ya Kikatoliki nchini Tanzania, Padri Charles Kitima ambaye amelazwa Hospitali ya Aga Khan kutokana na kujeruhiwa kichwani.

Dar es Salaam. Chama cha ACT Wazalendo kimelaani kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima wakitaka hatua za haraka kwa wahusika tukio hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Padri Kitima ameshambuliwa usiku wa jana Jumatano, Aprili 30, 3035 eneo la Kurasini, Temeke jijini Dar es Salaam makao makuu ya ofisi za TEC.

Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Rauli Mahabi, mkazi wa Kurasini kwa mahojiano na Padri Kitima alipelekwa Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu baada ya kujeruhiwa kichwani na kitu butu.

Leo Alhamisi, Mei 1, 2025, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu ametoa taarifa kwa umma juu ya tukio hilo akisema: “Tukio la kuvamiwa na kushambuliwa kwa kiongozi huyu wa dini ni la kushtusha na kustaajabisha na linatoa taswira mbaya na ya hatari juu ya hali ya usalama katika nchi yetu.”

“Inafikirisha, mtu wa kawaida anapata wapi ujasiri wa kuvamia na kumshambulia kiongozi wa dini aina ya Padre Kitima katika eneo la ofisi za TEC ambazo zina ulinzi wa kutosha katika kipindi hiki ambacho kiongozi huyo amekuwa sauti isiyotetereka ya kukemea maovu na ukiukaji wa haki unaotendeka nchini? ACT Wazalendo tunalaani vikali tukio la kushambuliwa kwa Padre Kitima.


“Shambulio lake ni ishara kuwa sasa hakuna aliye salama katika nchi yetu, vilevile ni ishara ya kushindwa kwa mamlaka zenye wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wetu. Tunahitaji kuona hatua za haraka zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika na kitendo hiki wakichukuliwa hatua za kisheria,” amesema Semu na kuongeza:

“Aidha, vitendo vya namna hii vikomeshwe kwani vinavunjavunja na kuondoa mshikamano, amani na utulivu wa kitaifa. Tunatumia fursa hii kumpa pole Padre Kitima na tunamuombea heri aweze kupona upesi na kurejea katika majukumu yake.”