Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Padri Kitima ashambuliwa, Polisi yamdaka mmoja

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima

Muktasari:

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, mtu huyo anashikiliwa na kuhojiwa ili hatua zichukuliwe.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Rauli Mahabi kwa tuhuma za kumjeruhiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima.

Hatua ya kushikiliwa kwa Mahabi mkazi wa Kurasini, Dar es Salaam, inatokana na taarifa za kushambuliwa kwa Padri Kitima iliyoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Padri Kitima ameshambuliwa eneo la Kurasini, Temeke jijini Dar es Salaam zilipo ofisi za TEC makao makuu.

Taarifa ya Polisi imetolewa leo, Alhamisi Mei 1, 2025 na Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro.

Katika taarifa hiyo, Muliro amesema Jeshi la Polisi linamshikilia na kumhoji Mahabi, mkazi wa Kurasini kuhusiana na tukio hilo.

"Anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika," ameeleza.

Kuhusu taarifa ilivyopokewa, Muliro amesema tukio hilo limetokea saa nne usiku wa kuamkia leo maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini, Temeke jijini Dar es Salaam.


"Padri huyo inadaiwa tangu saa tatu asubuhi (jana Jumatano) walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili," imeeleza taarifa ya Muliro.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Padri Kitima amepelekwa Hospitali ya Aga Khan na anaendelea na matibabu.

Endelee kufuatilia Mwananchi