Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

11 wafariki dunia ajalini Handeni, 13 wajeruhiwa

Handeni. Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo Kijiji cha Chang'ombe Kata ya Segera wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.

Ajali hiyo imetokea baada ya basi aina ya Tata kupinduka na baadaye wananchi kujitokeza kusaidia ndipo lori linalodaiwa kufeli breki likawagonga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 13, 2025 na kusema miili imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Korogwe.

Amesema tayari baadhi ya miili imeshatambuliwa na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu, huku taratibu za kusafirisha miili kwa gharama za Serikali ikiendelea.


Endelea kufuatilia Mwananchi