Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari watatu wafa ajalini

Muktasari:

  • Madaktari watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika kijiji cha Taula usiku wa kuamkia jana Alhamisi Novemba 21, 2019.

Handeni. Madaktari watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika kijiji cha Taula usiku wa kuamkia jana Alhamisi Novemba 21, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe amewataja madaktari hao kuwa ni Lazaro Zabron, Mussa Muro na Lucas Lubacha.
Alisema Dk Lucas Lubacha na Mussa Muro ni waganga wa kituo cha afya Mkata na Lazaro Zabron ni kutoka kituo cha afya Kabuku.
Makufwe alisema ajali hiyo ilitokea saa 4 usiku wakiwa wanatoka semina ya kikazi Moshi.
Alisema madaktari hao walipanda basi la kwenda Tanga mjini na walipofika Segera walipanda lori kwenda vituo vyao vya kazi na ndio walipopata ajali na kufariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupinduka kwa gari aina ya  Volvo.
"Ni kweli madaktari watatu wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kumkia leo ila mpaka sasa tunafuatilia kujua chanzo cha tukio kwani hakuna mtu aliyeshuhudia. Dereva wa gari hilo, Mohamed Bakari (29) yuko mahututi hospitali na utingo wake amefariki dunia," alisema Kamanda Bukombe.
Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya mji Handeni na mmoja katika hospitali ya Magunga iliyopo wilayani Korogwe.