Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wafariki ajalini Tanga

Muktasari:

  • Ndani ya wiki hii eneo hilo kumetokea ajali mbili zilizosababisha vifo vya watu watano na kujeruhi sita.

Handeni. Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika kata ya Kwedizinga wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga baada ya gari aina ya Toyota Hiace kuligonga lori.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Sofia Jongo amesema tukio lilitokea saa 12 asubuhi, leo Jumatano Septemba 7, 2022 ambapo hiace ilikuwa ikijaribu kupita lori eneo ambalo alama haziruhusu kupita hali ambayo dereva alishindwa na kuligonga lori hilo.

Amesema gari aina ya Toyota Hiace lilikuwa likijaribu kupita lori ambapo dereva alishindwa kasi na kujikuta analigonga lori hilo kwa nyuma, na kusababisha kifo cha dereva wa Hiace na abiria wake mwingine.

"Dereva huyo aliwapita polisi akiwa na mwendo wa kawaida ila mbele kumbe aliongeza mwendo na kusababisha kutokea ajali wakiwa wanapanda mlima uliopo eneo hilo ambalo kuna kona kali," amesema Kamanda Jongo.

Amesema eneo hilo hutokea ajali za mara kwa mara kwasababu watumiaji wa barabara wamekuwa wakitii sheria wanapoona polisi, ila walipoona dalili za uwepo wao huendesha kwa kasi na kupitana hali inayosababisha ajali za mara kwa mara.

Kamanda Jongo alisema madereva wanatakiwa kuwa makini kwenye eneo hilo la Kwedizinga kwani tete kutokana na kuwepo kona kali, lakini watumiaji wengine wa barabara wawe makini kwa kukemea mwendo kasi.