Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Vijana wanaongoza tatizo la afya ya akili, msongo wa mawazo’

Mwenyekiti wa umoja wa The Boost Community ambao ni Mabalozi wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk Martine Kayuli akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa umoja huo kwenye Hospitali ya Mirembe ambapo wametoa msaada wa kompyuta nane.

Muktasari:

  • Mabalozi wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe wametoa msaada wa kompyuta nane hospitalini hapo ili ziweze kurahisisha utendaji kazi.

Dodoma. Kundi la vijana la The Boost Community ambao ni Mabalozi wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe wametoa msaada wa vitendea kazi hospitalini hapo ikiwa ni juhudi zao za kuhakikisha hospitali hiyo inatoa huduma bila changamoto zozote.

Msaada uliotolewa leo Jumanne Septemba 26, 2023 ni kompyuta nane ambazo kundi hilo limezinunua kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya hospitalini hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakari Zubeir aliyewakilishwa na Shekhe Ally Ngeruko.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mabalozi hao Mwenyekiti wa kundi hilo, Dk Martin Kayuli amesema lengo la kuanzishwa kwa kundi hilo ni kuwasaidia vijana kuwezeshana kiuchumi pamoja na kutatua changamoto za kimaisha  zinazowakabili kwa njia salama.

Amesema vijana ndiyo waathirika wakubwa wa afya ya akili kulingana na takwimu zilizopo nchini kutokana na msongo wa mawazo, matumizi ya madawa ya kulevya na ugumu wa maisha ambao husababisha baadhi yao kujiua.

Amesema kundi hilo limeanzishwa ili kuwasaidia vijana wenzao wenye changamoto mbalimbali na kushauriana kuhusu masuala mbalimbali ya maisha kwenye furaha na kwenye huzuni.

"Vijana wengi wanapitia changamoto mbalimbali ambazo wanahitaji msaada, sasa wakikutana na vijana wenzao ambao hawana afya ya akili ndipo madhara yake yanaanza kuonekana hivyo sisi tumejiunga ili kuzitatua changamoto hizo pamoja na za wenzetu watakaotukimbilia," amesema Dk Kayuli.

Amesema umoja huo una jumla ya wanachama 47 ambao wanajishughulisha na majukumu mbalimbali za kiuchumi lengo ni kuhakikisha kuwa kila kijana anapata mahitaji yake ya muhimu kwa kufanya kazi iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri ili kupunguza msongo wa mawazo unaweza kusababisha ugonjwa wa akili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe, Dk Paulo Lawala amewapongeza vijana hao kwa uthubutu walioufanya na kuwataka kuwa mabalozi wema wa hospitali hiyo ili kushirikiana na serikali kutoa elimu ya afya ya akili kwa jamii.

Amesema hospitali hiyo inawahitaji watu kama hao ambao wana utayari wa kutoa elimu kuhusu afya ya akili kwa jamii ili wawe na uelewa mpana kuhusu elimu hiyo ambayo hivi sasa ndiyo kipaumbele cha Hopitali ya Mirembe.

Naye Mwenyekiti wa Maarifa ya Uislam (Juakita)  Mkoa wa Geita, Nurrath Hassan amewataka vijana wenye changamoto za afya ya akili kufika hospitalini hapo kwa ajili ya ushauri wa wanasaikolojia na matibabu ili waweze kurejea kwenye hali zao za kawaida.

Amelipongeza kundi hilo kwa kuona kuwa afya ya akili ni mtaji mkubwa kwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa hivyo wapewe kipaumbele kwenye elimu ya kujitambua na matibabu hayo.