Samia: Sekta ya anga tunasuasua, lakini tulipo siyo sawa na tulikotoka

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa sekta ya usafiri wa anga imeendelea kukua katika kipindi chake cha uongozi, licha ya changamoto kadhaa, kutokana na jitihada za kuifanya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kujiendesha kibiashara.
“Katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga, niliahidi kuendelea kuiboresha kampuni yetu ya ndege ATCL kimkakati ili iweze kujiendesha kwa ufanisi. Katika kipindi hiki, Serikali imenunua ndege 6 za abiria na moja ya mizigo, hivyo kufanya ATCL kuwa na jumla ya ndege 16. Hii imefanya usafiri wa ndani kuwa wa uhakika.
Ingawa bado tunasuasua, lakini tulipo si tulikotoka,” amesema Rais Samia.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 27, 2025, wakati Rais Samia anahitimisha shughuli za Bunge la 12, jijini Dodoma.