Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgogoro familia ya Marealle ngoma nzito

Paroko wa Parokia ya Samanga, Padri Ephurerm Mapendano (kulia) akimskiliza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Moshi, Joseph Kate (katikati) akisoma ujumbe wa kwenye simu wa wakuzuiya padre huyo asiendelee na ibada ya kumzika Veronica Marealle, kutokana na ndugu mmoja wa marehemu kupinga maziko yasifanyike katika makaburi ya familia katika Kijiji cha Lyamrakana, Marangu. Ujumbe huo ulitoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira. Picha na Dionis Nyato

Moshi. Mfanyabiashara Frank Marealle leo anatarajia kuwasilisha maombi mahakamani, kutaka mwili wa marehemu Veronica Marealle (105) uondolewe mahali ulipozikkatika eneo ambalo lina mgogoro.

Wakili wa mfanyabiashara huyo, Modestus Njau amesema awali maombi yao yalikuwa ni kuzuia mwili huo kuzikwa katika eneo analodai ni la mteja wake, jambo ambalo haliwezekani kwa kuwa tayari wameshazika.

Mwili wa mwanamke huyo ambaye alikuwa ni mke wa sita wa Mangi Marealle II, ulizikwa Jumamosi iliyopita katika kitongoji cha Moori, Kijiji cha Lyamrakana, katika maziko yaliyosimamiwa na polisi.

Pamoja na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Anna Mgh’wira kupeleka ujumbe mfupi (sms) kupitia kwa mkuu wa polisi wa wilaya ya Moshi (OCD), kuwa mazishi yaahirishwe au marehemu azikwe katika eneo lisilo na mgogoro, bado mazishi yalifanyika.

Maombi hayo namba 76 ya 2020 yaliyofunguliwa na Frank katika Baraza la Ardhi na Nyumba Moshi chini ya hati ya dharura, yamepangwa kusikilizwa leo na mwenyekiti wa baraza hilo, Silas James.

“Ili tuweze kuzungumza kesho (leo) mimi nitakuja na hoja moja kwamba inabidi baraza hilo hilo lirudishe status quo ante (hali kabla ya mazishi) ili tuweze sasa kuingia kwenye mjadala,” alidai wakili Njau.

“Jeneza litoke pale ndio tuzungumze wana haki ya kuzika wapi. Wazike popote lakini sio pale,” alisisema Njau.

“RC alitoa amri kupitia kwa OCD lakini mapolisi wakaona hawana order ya mahakama ya kuzuia (Veronica) asizikwe pale. Hilo likawafanya wasizuie,” alisema Njau.

“Kwa upande wa Polisi tulifungua shauri la kuingia kwa jinai katika hilo eneo lakini wakawa wazito kuzuia mtu asizikwe kwenye eneo la mwenzake, wao wakaamua kuzika palepale panapobishaniwa.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni, alisema waliamua kupeleka askari katika eneo hilo kwa ajili ya usalama, baada ya kuonekana viashiria vya kutokea jinai.

Acley Marealle ambaye ni mtoto wa marehemu na mjibu maombi katika kesi hiyo, alisema hakuna mahali walipokosea, kwa kuwa haikuwapo amri ya mahakama ya kuzuia maziko.