Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Dodoma mbona safi tu kwa maghorofa’

Muktasari:

Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya wananchi kuelekezea hofu yao kupitia mitandao ya jamii juu ya kuwekeza majengo mjini Dodoma ambao miongoni mwa mikoa ambayo Bonde la Ufa linapita.

 

Dodoma. Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) umewaondoa hofu wawekezaji wa majengo mjini Dodoma ukisema wanaweza kujenga maghorofa ilimradi wafuate taratibu zinazotumika ‘Building code’ zinazohusisha kupanga, michoro ya jengo na ufuatiliaji.

Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya wananchi kuelekezea hofu yao kupitia mitandao ya jamii juu ya kuwekeza majengo mjini Dodoma ambao miongoni mwa mikoa ambayo Bonde la Ufa linapita.

Meneja wa Jiolojia, Maruvuko Msechu amesema ni vyema kutafuta ushauri wa watalaamu kabla ya kuwekeza katika miradi akisema hiyo si kwa Dodoma pekee, bali nchini kote kwa sababu tetemeko linaweza kutoa eneo lolote.

Amesema matetemeko yanaweza kutokea mahali kokote nchini hata kama katika eneo hilo Bonde la Ufa halipiti.

Hata hivyo, amesema maeneo linakopita bonde hilo kama Mkoa Kagera ambako kulitokea tetemeko liliopoteza maisha ya watu 17 na wengine 250 kujeruhiwa, ni harari zaidi.

Msechu amesema matetemeko yataendelea kutokea na kwamba jambo muhimu ni kuchukua tahadhari kabla ya ujenzi wa majengo kwa kuhakikisha wahusika wanafuata ushauri wa kitaalamu.

“Hata hao wanaolala nje ya nyumba (Kagera) si ufumbuzi wa tatizo. Wanachotakiwa kufanya sasa hivi ni kufanya tathmini ya tukio lilojitokeza,” amesema.