Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaodaiwa kufanya uharifu shamba la Kenyatta wadakwa

Muktasari:

  • Japokuwa mamlaka za Kenya hazijabainisha idadi kamili ya washukiwa hao lakini imethibitisha kukamatwa kwao baada ya kusakwa kwa zaidi ya miezi kadhaa. Tovuti ya Tuko ya nchini humo imeripoti.

Kenya. Kama unakumbuka Machi mwaka huu zilisambaa taarifa za kundi la watu kuvamia, kuiba mifugo na kufanya uharibifu mkubwa kwenye shamba la aliyekuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta sasa mamlaka za nchini humo zimetangaza kukamatwa kwa watu hao.

Ikiwa imepita miezi mitatu tu, Waziri wa Usalama wa Kenya Kithure Kindiki amethibitisha kukamatwa kwa washukiwa hao walioiba kila kitu na kuliacha shamba likiwa linateketea kwa moto huku wengine wakionekana wakiwabeba kondoo mabegani na kutokomea nao.

Kindiki amebainisha hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari katika ofisi yake jijini Nairobi ingawa hajatoa maelezo kamili kuhusu idadi kamili ya washukiwa walio kamatwa.

"Kile kilichotokea Northlands ni uhalifu mkubwa. Tumefanya uchunguzi na hivi karibuni tutawashtaki baadhi ya washukiwa. Imechukua muda kidogo kutokana na tukio hilo kuchochewa kisiasa," alisema Kindiki.

Ikumbukwe uvamizi katika shamba la hilo lililopo karibu na barabara ya Eastern bypass ulitokea Machi 27, 2023, ambapo watu hao walijihami na mapanga na mashine ya kukata miti, walivunja uzio na kuingia katika shamba hilo kubwa kabla ya kuiba kondoo na kulichoma moto.