Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya Marekani, Iran bado kaa la moto, Trump aweka ngumu

Rais wa Marekani, Donald Trump

Muktasari:

  • Usitishaji wa vita kati ya Iran na Marekani imeendelea kuchukua sura mpya baada ya Trump kujibu na kuyakataa mapendezo yao.

Marekani. Rais wa Marekani, Donald Trump amesema usitishaji wa mapigano wa mwezi mmoja kati ya Marekani na Iran uko katika hali ‘mahututi’, huku akionya kuwa mvutano kati ya mataifa hayo mawili unaweza kuongezeka tena.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval usiku wa Jumatatu Mei 11, 2026, Trump amesema ingawa makubaliano hayo bado hayajavunjika rasmi, hali yake imeendelea kuwa dhaifu.

“Ningesema usitishaji mapigano uko katika hali mbaya. Ni kama daktari anapoingia na kusema mgonjwa ana nafasi ya asilimia moja pekee ya kuendelea kuishi,” amesema Trump.
Rais huyo pia amewashutumu viongozi wa Iran kwa kile alichodai ni kubadilisha misimamo mara kwa mara katika mazungumzo yanayoendelea.

“Huo upuuzi waliotutumia hata sikuumaliza kuusoma,” amesema.
Trump ameendelea kuishutumu Tehran kwa madai ya kuvunja makubaliano ya kuruhusu Marekani kuondoa akiba ya urani iliyorutubishwa, akisisitiza kuwa Iran haitaruhusiwa kumiliki silaha za nyuklia.

Moja ya milipuko iliyotokea katika mji wa Iran kutokana na vita ya Marekani. Picha na Mtandao

Kauli hizo zimekuja saa chache baada ya Iran kuwasilisha mapendekezo yake ya kusitisha vita na kufunguliwa tena kwa Mlango wa Hormuz kupitia ofa mbadala iliyowasilishwa kwa Marekani Jumapili.

Hata hivyo, Trump aliyakataa mapendekezo hayo, akiyataja kuwa hayakubaliki na kuyataja kama ni upuuzi.

Kufuatia matamshi hayo, Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Ghalibaf ameandika katika mtandao wa X kuwa majeshi ya Iran yako tayari kujibu na kutoa funzo kwa uchokozi wowote utakaoibuka.

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Ghalibaf

Kwa upande wake, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema mapendekezo yao yalikuwa ya uwajibikaji na ukarimu.

Baadaye, Ghalibaf alisema hakuna njia nyingine isipokuwa kukubaliwa kwa haki za wananchi wa Iran kama zilivyoainishwa katika pendekezo la vipengele 14.

“Kadri wanavyoendelea kuchelewesha, ndivyo walipa kodi wa Marekani watakavyozidi kulipa gharama kubwa,” amesema.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim News Agency, pendekezo la Iran linajumuisha kusitishwa mapigano katika maeneo yote yenye migogoro, kuondolewa majeshi ya Marekani kuzingira baharini dhidi ya bandari za Iran pamoja na dhamana ya kutofanyika mashambulizi dhidi ya taifa hilo.

Trump alijibu kupitia mtandao wake wa Truth Social akisema:

“Nimesoma majibu kutoka kwa wanaojiita wawakilishi wa Iran. Siyapendi kabisa, hayakubaliki kabisa,”
Akijibu kauli hizo, Baghaei amesema Iran iko tayari kuchukua hatua kwa njia yoyote itakayohitajika kulinda maslahi yake.


Imeandikwa kwa msaada wa Mashirika.