Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpango wa Trump kupunguza fedha za afya duniani wazua hofu

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na CNN, fedha hizo zilikuwa zimeidhinishwa na Bunge la Marekani kusaidia mapambano dhidi ya malaria, kifua kikuu (TB), VVU/Ukimwi, lishe kwa watoto na kina mama, pamoja na usalama wa afya duniani.

Serikali ya Rais Donald Trump inapanga kuelekeza upya zaidi ya dola bilioni mbili za Marekani zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya programu za afya duniani ili kufidia gharama za kufungwa kwa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hatua iliyozua hofu kubwa kwa wataalamu wa afya duniani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na CNN, fedha hizo zilikuwa zimeidhinishwa na Bunge la Marekani kusaidia mapambano dhidi ya malaria, kifua kikuu (TB), VVU/Ukimwi, lishe kwa watoto na kina mama, pamoja na usalama wa afya duniani.

Mpango huo pia unahusisha kuelekeza upya dola bilioni 1.2 zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya misaada ya maendeleo ya kimataifa.

Badala yake, fedha hizo zinatarajiwa kutumika kugharamia madeni ya kisheria, bili mbalimbali na uuzaji wa mali kufuatia hatua ya serikali ya Trump kuivunja USAID na kuhamishia baadhi ya programu zake chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Mwaka jana, utawala wa Trump ulisitisha kwa muda karibu misaada yote ya nje na kufuta maelfu ya mikataba ya misaada, hatua iliyotikisa sekta ya misaada ya kibinadamu duniani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali ya Marekani imeitaarifu Congress kuwa imetenga zaidi ya dola bilioni 19.1 kwa ajili ya gharama za kufunga shughuli za USAID.

Hatua hiyo imezua upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge wa chama cha Democratic. Kundi la maseneta 17 limetaka serikali ya Trump kufuta mpango huo na kurejesha fedha hizo katika matumizi yake ya awali ya kuokoa maisha.

Katika barua yao kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, wabunge hao wamesema hakuna sababu ya fedha za misaada ya afya kuzuiliwa ili kufidia gharama zilizotokana na uamuzi wa kuivunja USAID.

Wataalamu wa sera za afya wameonya kuwa kupunguzwa kwa fedha hizo kunaweza kusababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.

Tathmini ya taasisi ya Health Security Policy Academy inaonyesha kuwa kupunguzwa kwa dola bilioni mbili kunaweza kusababisha vifo vinavyoweza kuzuilika vya watu zaidi ya 121,000 kutokana na kifua kikuu na wengine 47,600 kutokana na malaria.

Aidha, wataalamu wameonya kuwa mamilioni ya watoto wanaweza kukosa huduma muhimu za lishe huku wanawake zaidi ya milioni 5.7 wakikosa huduma salama za uzazi.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo misaada ya afya duniani imekuwa ikipungua kutoka kwa nchi mbalimbali wafadhili.

Katika maendeleo mengine, wachambuzi wa sera za afya wameeleza wasiwasi wao kuhusu matumizi hafifu ya fedha za mpango wa Marekani wa kupambana na VVU/UKIMWI duniani wa PEPFAR.

Mpango huo ulianzishwa mwaka 2003 chini ya utawala wa George W. Bush na umehusishwa na kuokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 26, hasa barani Afrika.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema takribani dola bilioni 1.7 zilizokuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya programu hiyo bado hazijatumika, huku sehemu ya fedha hizo ikiwa haijapelekwa hata kwa taasisi zinazotekeleza huduma hizo.

Mashirika ya kutetea afya duniani yameonya kuwa hatua hizo zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mingi katika mapambano dhidi ya VVU, kifua kikuu na malaria, hasa katika nchi zinazoendelea barani Afrika.

Ripoti mpya zinaonyesha kuwa idadi ya vipimo vya VVU vilivyofadhiliwa na PEPFAR ilipungua kwa vipimo milioni 14 mwaka 2025, sawa na upungufu wa asilimia 17 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Wataalamu wa afya wameonya kuwa kupungua kwa vipimo kunamaanisha watu wengi wanaweza wasigunduliwe mapema na kupata matibabu.

“Ukiona idadi ya watu wanaopimwa inapungua, inaonyesha kuna watu wanakosa kugundulika,” amesema Jennifer Kates, mtaalamu wa sera za afya duniani.

Naye Charles Kenny amesema kupunguzwa kwa huduma za jamii na kufutwa kwa ma