Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unicef yataka suluhu mapigano Israel, Palestina kuwanusuru watoto

Muktasari:

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto Duniani (Unicef), Catherine Russell imetaka kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea Israel na Palestina ili kuwanusuru watoto.


New York.  Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto Duniani (Unicef), Catherine Russell imetaka kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea Israel na Palestina ili kuwanusuru watoto.

"Unicef inataka kusitishwa mara moja kwa uhasama, na kwa pande zote kuwalinda watoto dhidi ya madhara na kuwapa ulinzi maalumu ambao wanastahili kupata, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu,” ameeleza taarifa hiyo kupitia ukurasa wa shirika hilo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Unicef inajali ustawi wa watoto wa Israel na Palestina na wanafuatilia kwa karibu hali ilivyo, kuripoti ukiukwaji mkubwa wa haki zinazofanywa dhidi ya watoto, pamoja na raia wanaoripotiwa kuuawa au kujeruhiwa.

"Zaidi ya yote, wana wa Israeli na Palestina wanahitaji suluhisho la kudumu la kisiasa kwa mgogoro huo, ili waweze kukua kwa amani na bila kivuli cha vurugu," amesema.

Taarifa zinasema maelfu ya watu wameshapoteza maisha na wengine kujeruhiwa tangu kuanza kwa mapigano hayo mapema Jumamosi.


Imeandikwa na Sute Kamwelwe kupitia Mashirika ya Kimataifa